logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Fahamu jinsi ya kuripoti tatizo la kukatika kwa umeme kwa Kenya Power

Wateja wa Kenya Power wanaweza kuripoti hitilafu ya umeme kwa urahisi kupitia simu zao za mkononi.

image
na Samuel Mainajournalist

Yanayojiri25 March 2025 - 08:06

Muhtasari


  • Kwa wale wanaokumbwa na changamoto za umeme, kuna njia mbili kuu za kuripoti: Kupiga *977# au kutumia myPower App.
  • Kenya Power inasema kuwa huduma hii inalenga kuboresha ufanisi wa kushughulikia changamoto za umeme kwa haraka.

Kenya Power staff

Wateja wa Kenya Power wanaweza kuripoti hitilafu ya umeme kwa urahisi kupitia simu zao za mkononi. Kampuni hiyo imebuni njia rahisi na za haraka kuhakikisha malalamiko yanashughulikiwa kwa wakati.

Kwa wale wanaokumbwa na changamoto za umeme, kuna njia mbili kuu za kuripoti: Kupiga *977# au kutumia myPower App, inayopatikana kwenye App Store na Google Play Store.

"Tunapopokea malalamiko ya wateja, tunajitahidi kutoa suluhisho la haraka au kutoa nambari ya kumbukumbu kwa ufuatiliaji ndani ya muda uliowekwa wa utatuzi," Kenya Power ilieleza kupitia chapisho la video kwenye kurasa zake rasmi za mitandao ya kijamii.

Katika taarifa yake, kampuni hiyo ya kusambaza umeme nchini ilieleza mchakato wa kupiga ripoti hatua kwa hatua.

Jinsi ya Kuripoti Tatizo Kupitia 977#

1. Piga *977# kwenye simu yako.

2. Chagua ‘Report Incidences’ (Ripoti Tukio).

3. Chagua aina ya tatizo unalotaka kuripoti.

4. Chagua aina ya akaunti (Prepaid/Postpaid)

5. Weka nambari ya akaunti yako.

6. Chagua sababu ya tukio kisha tuma.

7. Utapokea nambari ya kumbukumbu kwa ajili ya ufuatiliaji.

Kenya Power inasema kuwa huduma hii inalenga kuboresha ufanisi wa kushughulikia changamoto za umeme kwa haraka.

Kwa sasa, kampuni hiyo inahudumia zaidi ya wateja milioni 9.6 kote nchini, huku ikitoa chaguo la akaunti mbili kuu—Prepaid na Postpaid—kulingana na mahitaji ya kila mteja.

Kila wiki na kila siku, Kenya Power hutoa taarifa ikiwaonya wateja wake kuhusu maeneo yatakayoathiriwa na kukatika kwa umeme kulikopangwa kote nchini.Kukatika huku kwa umeme kwa kawaida hutokana na ukarabati unaoendelea.

Jioni ya Jumatatu, kampuni hiyo ilitoa tahadhari kwamba maeneo kadhaa katika kaunti saba yatakumbwa na hitilafu ya umeme Jumanne, Machi 25, 2025.

Kaunti zitakazoathirika ni Nairobi, Nandi, Elgeyo Marakwet, Kiambu, Trans Nzoia, Kisumu, na Kirinyaga.

Makala Zinazohusiana


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved