logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Mwanamke wa Kenya akamatwa na Kokeini ya mamilioni ya pesa nchini India

Dawa hiyo inakadiriwa kuwa ya thamani ya Sh.273 milioni hadi Sh.364 milioni.

image
na Samuel Mainajournalist

Yanayojiri03 April 2025 - 13:24

Muhtasari


  • Mshukiwa alidaiwa kuhusika katika usafirishaji haramu wa 1.7kg ya cocaine kutoka Nairobi kupitia Doha.
  • Uchunguzi wa mizigo yake ulibaini kuwepo kwa pakiti nne zilizo na dawa za kulevya.

CRIME SCENE

Maafisa wa forodha katika uwanja wa ndege wa Mumbai, nchini India mnamo Jumanne, Aprili 1, walimkamata Emily Kannin Rodha, mwanamke wa Kenya mwenye umri wa miaka 43, ambaye alidaiwa kuhusika katika usafirishaji haramu wa 1.7kg ya cocaine kutoka Nairobi kupitia Doha.

Kwa utekelezaji wa taarifa maalum, ofisa walimkamata Rodha alipofika uwanjani wa ndege ya Chhatrapati Shivaji Terminals jijini Mumbai.

Waliripoti kuwa alifika uwanjani kupitia Doha.

Uchunguzi wa mizigo yake ulibaini kuwepo kwa pakiti nne zilizo na unga, na majaribio kwa kutumia kifaa cha uchunguzi cha uwanja yalithibitisha kuwa dawa hiyo ni cocaine.

Wataalam wamehesabu uzito wa dawa hizo kuwa gramu 1,789, na thamani yake inakadiriwa kuwa kati ya Rs 15 hadi 20 crores.

Kutumia kiwango cha ubadilishaji cha 1 INR = 1.82 KES, thamani hiyo inafikiriwa kuwa Sh.273 milioni hadi Sh.364 milioni, kulingana na ubora wa cocaine iliyopatikana.

Hatua hii imetathminiwa kuwa hatua muhimu katika juhudi za kupambana na biashara haramu ya dawa za kulevya na kuhakikisha usalama katika viwanja vya ndege vya kimataifa.


Makala Zinazohusiana


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved