
KAMPUNI ya kusambaza umeme nchini Kenya (KPLC) imeonya kuhusu kukatizwa kwa umeme katika maeneo kadhaa nchini siku ya Jumatatu, Aprili 14.
Katika taarifa ya Jumapili jioni, kampuni hiyo ilisema kukatizwa kwa umeme kutatokana na ukarabati ambao utakuwa ukifanyika kwenye mitambo.
Walisema baadhi ya maeneo ya kaunti saba za Kenya yatakosa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi na moja jioni.
Kaunti ambazo zitaathirika ni pamoja na Nairobi, Kakamega, Trans Nzoia, Meru.
Katika kaunti ya Nairobi, sehemu za eneo la Galleria Mall zitaathirika na kukatizwa na umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi na moja jioni.
Maeneo ya Makutano na Ivona katika kaunti ya Kakamega yataathirika kati ya saa mbili asubuhi na saa kumi na moja jioni.
Sehemu za maeneo ya Kapsara, Ngonyek, na Sibanga katika kaunti ya Trans Nzoia zitakosa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi na moja jioni.
Katika kaunti ya Meru, sehemu za maeneo ya Rubiri Kaubau na Kagwampugu zitakosa umeme kati ya saa mbili unusu na saa kumi na moja jioni.