
Rais Ruto Jumatano ya tarehe 16 Aprili, 2025 aliwarai viongozi, wanasiasa kutoingiza siasa katika masual ya jeshi
Rais Ruto alikuwa akizungumzia hayo alipokuwa Lanet akizindua hospitali ya ukanda huo wa Nakuru. Rais alizungumzia suala la jeshi la ulinzi la taifa akisema kuwa hatakubali viongozi, wanasiasa au vyombo vya habari kuweza kuliingiza jeshi katika masuala ya siasa.
Kiongozi wa taifa alisema hayo akirejelea matukio ya hapo awali ambapo viongozi wa kisiasa pamoja na vyombo vya habari viliweza kuchapisha habari kuhusu jeshi la nchi. Hio ilifuatia kuwa kulikuwa na mkengeuko wa kizazi cha sasa cha GEN Z ambapo mara kwa mara wamekuwa
Kiongozi wa taifa alisema hayo akirejelea matukio ya hapo awali ambapo viongozi wa kisiasa pamoja na vyombo vya habari viliweza kuchapisha habari kuhusu jeshi la nchi.
Hio ilifuatia kuwa kulikuwa na mkengeuko wa kizazi cha sasa cha GEN Z ambapo mara kwa mara wamekuwa
wakimshutumu kwa kusema kuwa ni lazima aende alimaarufu ''Ruto must Go'' Jambo ambalo lilichochea usimamizi na viongozi wa ngazi za juu za usalama kutoa kauli zao.
Kiongozi wa kitengo cha ujasusi Nurdin Haji na Mwenzake mkuu wa majeshi Charles Kahariri waliweza kuonya umma dhidi ya kutumia uhuru wao wa mitandao kuweza kulitumbikiza taifa katika hali ya mapinduzi au kuharibu taifa kwa masuala ya kibinafsi.
Ni kutokana na matukio hayo ambapo rais alitoa onyo kuhusu kuliingiza jeshi kwenye masuala ya siasa.
'' Kwa maendeleo ya kitaifa hujengwa kwa misingi ya amani uongozi mwema na ujumuishaji wa kila mmoja katika ufanikishaji wa maendeleo ya taifa. "
"Vikosi vyetu vya usalama wa jeshi viko imara kwa kuhakikisha kuwa vinatimiza haya malengo na matakwa kwa hivyo kuwepo kwao ni kujihakikishia kuwa kunakuwa na usimamizi imara ambapo husaidia kuwavutia wawekezaji na huchochea uhusiano mzuri wa nchi na wa kimataifa."
"Kwa hivyo ningependa kurai kila Mkenya, viongozi, wanasiasa na vyombo vya habari kuwa jeshi letu likijumuisha akina dada na kaka zetu hao ndio nguzo imara na muhimu katika kuendelea na ustawi wetu kama taifa."
"Hakikisha kuwa lazima tuwe imara na tuweze kuwa makini na kuweza kujiepusha na kuzungumzia jeshi kwa ubaya wowote ule, serikali yangu itajitolea kwa hali na mali kuhakiksha kuwa inalinda jeshi la taifa bila uwoga wala shauku yoyote '' Rais Ruto alisema.