logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Kenya Power yatangaza maeneo ambayo yatakosa umeme leo, Alhamisi

Kaunti zitakazoathirika ni Nairobi, Kajiado, Uasin Gishu, Kakamega, Meru, Kiambu na Mombasa.

image
na Samuel Mainajournalist

Yanayojiri17 April 2025 - 07:26

Muhtasari


  •  Kenya Power imetangaza kuwa maeneo kadhaa katika kaunti saba yataathirika na kukatika kwa umeme siku ya Alhamisi.
  • Umeme utakatwa kuanzia saa tatu asubuhi hadi saa kumi na moja jioni katika maeneo yaliyoorodheshwa.

Kenya Power technicians at work

Shirika la Kenya Power limetangaza kuwa maeneo kadhaa katika kaunti saba yataathirika na kukatika kwa umeme siku ya Alhamisi, kutokana na matengenezo ya kawaida na kazi za kuboresha huduma.

Kaunti zitakazoathirika ni Nairobi, Kajiado, Uasin Gishu, Kakamega, Meru, Kiambu na Mombasa. Umeme utakatwa kuanzia saa tatu asubuhi hadi saa kumi na moja jioni katika maeneo yaliyoorodheshwa.

Katika jiji la Nairobi, maeneo yatakayoathirika ni General Mathenge Drive, Mpaka Road, sehemu za 2nd na 3rd Parklands, Eldama Ravine, Suswa Road, Kusi Lane pamoja na maeneo jirani.

Katika Kaunti ya Kajiado, maeneo yatakayokosa umeme ni St. Patrick, Barabara ya Mwalimu, Oleteyani, Ilmasin, Olooses, Kisamis, Homeboys, Lingaloj, Ilidoriak, Tinga, Esonorua Matasia, Nkoroi, Olesurutia, Barabara ya Tajiri, Merisho na vitongoji vya karibu.

Uasin Gishu nayo itaathirika katika maeneo ya Mbingwa, Ivigwa, Sango, Likuyani, Frank na Lugulu.

Kwa upande wa Kaunti ya Kakamega, maeneo kama vile Soko la Butere, Soko la Shashiala, Maondo, Khomailo, Mapole, Soko la Eshishiebo na Soko la Emanyulia yatapoteza umeme.

Katika Kaunti ya Meru, maeneo yatakayokumbwa na ukosefu wa umeme ni Nkoune, Shule ya Msingi ya Mwiriene, Chuo cha Walimu cha Meru, Shule ya Upili ya Mwithumwilu, Shule ya Upili ya Wasichana ya Kaaga, Kijiji cha Mpakone, eneo lote la Kaaga, Kituo cha Mafuta cha LR, Gatimene Gardens, Runogone, Chuo Kikuu cha KEMU, Tuliza FM, Gakurine, Kiandiu, Chungu, Soko la Kwiriro, Runogone Airtel, Soko la Kaithe, Kithoka, Freds Academy, Kituo cha Utamaduni cha Thiiri, Bishop Lawi, Shule ya Msingi na Sekondari ya Imathiu, Kithoka Ripples na maeneo ya karibu.

Katika Kaunti ya Kiambu, maeneo yanayotarajiwa kuathirika ni Shule ya Msingi ya Magajo, Farainya St. Paul Gatuanyaga, Shule ya Msingi ya Magana, Shule ya Wasichana ya Munyu, Zahanati ya Munyu, Kituo cha Polisi cha Munyu, Vituo vya biashara vya Githima na Komo, Juja Farm Athi, Kwa Ruhi, Juja Farm Mukuyu-Ini, Kwa Murage na maeneo jirani.

Maeneo mengine ya Kiambu yatakayokosa umeme ni Fresha Dairies, Palm House Dairies, County Pride, Thakwa, Wanjo, Maduka ya Githunguri, AP Canteen, Beta Care, Equity, kituo cha mafuta cha Shell Githunguri na maeneo ya karibu.

Hatimaye, katika Kaunti ya Mombasa, maeneo yatakayokumbwa na hitilafu ya umeme ni Husein Dairy, Kimbunga, Marimani, Voroni, Dampo la Mwakirunge, Shule ya Msingi ya Mwakirunge, Vifwanjoni, Bwagamoyo, KAA, John Ria pamoja na maeneo ya karibu.

Makala Zinazohusiana


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved