logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Mechi ya Uholanzi yasimamishwa baada ya kipa kupoteza fahamu

Wachezaji walitaka usaidizi kwa hamaki na walikuwa wakibubujikwa na machozi wakati Vaessen aliyekuwa kimya akipatiwa matibabu uwanjani.

image
na Samuel Maina

Michezo01 October 2023 - 14:37

Muhtasari


  • •Mchezo huo ulisimamishwa katika dakika ya 84 baada ya Mholanzi huyo, 28, kugongana na mshambuliaji wa Ajax, Brian Brobbey.

Mechi ya vinara wa Uholanzi kati ya RKC Waalwijk na Ajax iliachwa baada ya kipa wa Etienne Vaessen kupoteza fahamu.

Mchezo huo ulisimamishwa katika dakika ya 84 baada ya Mholanzi huyo, 28, kugongana na mshambuliaji wa Ajax, Brian Brobbey.

Wachezaji walitaka usaidizi kwa hamaki na walikuwa wakibubujikwa na machozi wakati Vaessen aliyekuwa kimya akipatiwa matibabu uwanjani, na skrini iliyowekwa ikionyesha kinachojiri.

Klabu yake ilisema alipata fahamu wakati akitolewa kwenye machela. RKC alisema: “Baada ya kufanyiwa uchunguzi wa kina wa kimatibabu amesafirishwa hadi hospitali kwa uchunguzi zaidi.

Ajax walikuwa wakiongoza mchezo wa Jumamosi wa Eredivisie kwa mabao 3-2 kabla ya mechi kusimamishwa.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved