
KUFUATIA kushindwa kwa timu yake na West Ham wikendi, mkufunzi wa Arsenal Mikel Arteta amejitokeza kupinga mapendekezo kwamba mbio za ubingwa zimekamilika.
Kupoteza huko pamoja na ushindi wa vinara Liverpool dhidi ya
Manchester City kunamaanisha kuwa Wekundu hao wanasalia kwa pointi 11 kabla ya
Machi (ingawa Arsenal wana mchezo mmoja mkononi).
Alipoulizwa iwapo anakubali taji hilo, jibu la Mhispania huyo
lilikuwa butu.
"Over my dead body!
Kama sitaamini [moyoni mwangu kwamba tunaweza kushinda] basi nitaenda
nyumbani," alisisitiza.
"Kihisabati
inawezekana, upo na lazima ucheze kila mchezo. Siku tatu zilizopita tungeweza
kufunga pengo halafu umebakisha mechi moja na nusu.”
"Haijalishi. Lazima
tuendelee. Huu ndio ugumu. Ni ngumu zaidi ya siku tatu zilizopita lakini kama
unataka kushinda Ligi Kuu, katika mazingira tuliyo nayo, lazima ufanye kitu
maalum na ambacho hakuna mtu mwingine amefanya."
Licha ya wasiwasi kuwa kinara wa ujana Ethan Nwaneri
alitolewa katika kipigo na West Ham, Arteta pia alifichua kwamba hakuna sababu
ya kuwa na wasiwasi.
"Alikuwa anajikaza tu. Ilikuwa ni uchovu,"
aliongeza. "Ni wazi mzigo wake umekuwa tofauti sana na vile alivyozoea
katika wiki za hivi karibuni lakini yuko sawa." Ikiwa alikuwa akikubali
ubingwa, jibu la Mhispania huyo lilikuwa butu.