
NYOTA wa Liverpool, Mo Salah amepata ushindi mmoja zaidi dhidi ya Manchester United kwa kuwa 'mkubwa' kuliko wapinzani wao wa Reds' - kwenye Instagram.
Fowadi huyo wa Misri ana rekodi nzuri dhidi ya Mashetani
Wekundu, akiwa amefunga mabao 16 na kutoa asisti sita katika mechi 17
alizocheza dhidi ya Man Utd.
Na kutokana na mechi yake ya hivi majuzi dhidi yao ugani
Anfield mnamo Januari ambayo inaweza kuwa ya mwisho kwa mkataba wake
unaomalizika, Salah amewaletea pigo la mwisho wapinzani wa klabu yake.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 32 amewazidi wafuasi wa
United kwenye Instagram, akiwa na milioni 64.5, huku United wakiwa na 64.3m
pekee.
Bila kustaajabisha, mashabiki wa Liverpool waliochangamka
wamekuwa wepesi kupaka chumvi kwenye majeraha ya United.
Shabiki mmoja wa Liverpool aliandika: “Hakuna namna Salah ni
mkubwa kuliko Man United,” huku mwingine akisema: “Anamiliki Manchester United
ndani ya uwanja na nje yake”. Mashabiki wa United pia wametoa maoni yao, huku
wengine wakisema ukweli kwamba ameipita Liverpool.
"Ana wafuasi wengi kuliko Liverpool," shabiki mmoja
alisema, na mwingine akijibu: "Inamaanisha kuwa ana wafuasi wengi kuliko
klabu yake," pamoja na picha ya skrini inayoonyesha Liverpool ikiwa na
wafuasi 46.6m kwenye Instagram.
Salah hapo awali alielezea rekodi yake nzuri dhidi ya United
lakini akapendekeza asijitokeze kutafuta goli dhidi ya Mashetani Wekundu.
Akizungumza mwanzoni mwa msimu huu, alisema: "Naenda tu
kwenye mchezo, jaribu kuzingatia mchezo na kushinda mchezo.
Najua maana yake kwa mashabiki na jiji, kwa hivyo huwa
najaribu kusaidia timu na kufunga mabao. Tukifunga mabao tunayo nafasi nzuri ya
kushinda mchezo kwa hivyo huwa nazingatia mchezo, kujaribu kusaidia timu
kushinda mchezo."