
Mulamwah aliweka picha na video kwenye mitandao yake ya kijamii akiwa na mchezaji huyo ambaye ni mlinzi wa timu ya Arsenal.
"Hapa Dubai ni kutesa, nimekutana na kusalimiana na wachezaji wa Arsenal " Mulamwah aliandika kwenye mtandao wake wa Instagram.
"Team Arsenal gonga like..... ati anaitwa nani" aliandika baada ya kuweka picha na video alizopiga na watoto wa kizungu. Watoto wa kizungu waliitisha kupiga picha naye.
Mlamwa awali pia alikuwa ameweka video yake kabla ya kuwasili Dubai na kusema kuwa atakuwa huko kwa siku mbili na lengo lake ni kukutana na wachezaji wa Arsenal.
"Watu wangu ndo kuingia Dubai sasa kutoka mtaani na kuingia kukutana na wechezaji wa Arsenal. nitakutana na kusalimiana na wachezaji wa Arsenal, niktakutana na kina Saliba, zichenko, Martineli hao wote, niambie nini Saka," Mulamwah alisema kwenye video.
William Alain André Gabriel Saliba ni mchezaji wa soka wa Ufaransa ambaye anacheza kama beki wa kati wa klabu ya Ligi Kuu ya Uingereza Arsenal na vilevile timu ya taifa ya Ufaransa. mchezaji huyo ni mmoja wa mabeki bora wa kati ulimwenguni, anajulikana kwa nguvu , kasi, kukabiliana bila wasiwasi. kwa sasa ana umri wa miaka 24.
William Saliba ameichezea Arsenal kwa misimu mitatu kufikia sasa. Licha ya kuwa beki wa kati ana rekodi ya kufunga mabao 4, kusaidia mara 2, hajapoteza michuano mara 32 wakati akiwa kwenye mchezo. amehusishwa kwenye michuano 75 tangu kuwasili Arsenal. saliba amekinga mikwaju 4 ambayo ilikuwa karibu kufungwa.
Dubai ndio jiji lenye watu wengi zaidi katika Umoja wa Falme za Kiarabu na mji mkuu wa Emirates ya Dubai, jiji lenye watu wengi zaidi katika taifa hilo. Kufikia 2024, jiji lina idadi ya watu karibu milioni 3.79