logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Europa 2020/21: Usiku wa kusahau kwa Manchester United

Villarreal imeshinda kombe la Europa baada ya kuangusha mabingwa wawili wa Uingereza, Arsenal kwenye nusu fainali na klabu ya Manchester United kwenye fainali.

image
na Samuel Maina

Michezo27 May 2021 - 04:30

Muhtasari


  • •Villarreal imeshinda kombe la Europa baada ya kuangusha mabingwa wawili wa Uingereza, Arsenal kwenye nusu fainali na klabu ya Manchester United kwenye fainali.
  • •Ushindi wa Vilarreal ulihakikishia mkufunzi Unai Emery kombe lake la nne kwenye ligi hiyo.
Klabu ya Villarreal

Hatimaye ligi ya Europa msimu 2020/21 imefika tamati huku klabu ya Villarreal kutoka Uhispani ikibeba kikombe hicho.

Villarreal imeshinda kombe hilo kwa kuangusha mabingwa wawili wa Uingereza, Arsenal kwenye nusu fainali nayo klabu ya Manchester United kwenye fainali.

Mechi ya fainali kati ya Villarreal na Manchester United ilichezwa usiku wa Jumatano katika uwanja wa Stadion Miejski nchini Uholanzi.

Mechi hiyo iliisha sare ya 1-1 baada ya klabu ya Villarreal kufunga kwenye kipindi cha kwanza kupitia mchezaji matata Gerald Moreno nayo klabu ya Manchester United ikisawazisha kwenye kipindi cha pili kupitia mshambulizi Edinson Cavani.

Bao ya Cavani katika dakika ya 55 ilikuwa imerejesha matumaini ya klabu ya Manchester ambao ni mabingwa wa kombe hilo mwakani 2017 ila mechi hiyo ikaenda hadi kwa kwenye mikwaju ya penalti ambapo walipoteza vijana wa Ole Gunnar Solskjaer.

Mikwaju ishirini na moja ilifungwa huku Villarreal wakifunga 11 na Manchester United wakifunga 10 baada ya mlinda lango wake, David Degea kupoteza mukwaju wake na kuinyima klabu yangu kombe la pili la Europa.

Ushindi wa Vilarreal ulihakikishia mkufunzi Unai Emery kombe lake la nne kwenye ligi hiyo. Amefika fainali tano sasa huku akipoteza moja tu na klabu ya Arsenal mwakani 2019. Alishinda kombe tatu na klabu ya Sevilla mwakani 2014, 2015 n 2016.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved