HONGERA VILLARREAL !

Europa 2020/21: Usiku wa kusahau kwa Manchester United

Villarreal imeshinda kombe la Europa baada ya kuangusha mabingwa wawili wa Uingereza, Arsenal kwenye nusu fainali na klabu ya Manchester United kwenye fainali.

Muhtasari

•Villarreal imeshinda kombe la Europa baada ya kuangusha mabingwa wawili wa Uingereza, Arsenal kwenye nusu fainali na klabu ya Manchester United kwenye fainali.

•Ushindi wa Vilarreal ulihakikishia mkufunzi Unai Emery kombe lake la nne kwenye ligi hiyo.

Klabu ya Villarreal
Klabu ya Villarreal
Image: HISANI

Hatimaye ligi ya Europa msimu 2020/21 imefika tamati huku klabu ya Villarreal kutoka Uhispani ikibeba kikombe hicho.

Villarreal imeshinda kombe hilo kwa kuangusha mabingwa wawili wa Uingereza, Arsenal kwenye nusu fainali nayo klabu ya Manchester United kwenye fainali.

Mechi ya fainali kati ya Villarreal na Manchester United ilichezwa usiku wa Jumatano katika uwanja wa Stadion Miejski nchini Uholanzi.

Mechi hiyo iliisha sare ya 1-1 baada ya klabu ya Villarreal kufunga kwenye kipindi cha kwanza kupitia mchezaji matata Gerald Moreno nayo klabu ya Manchester United ikisawazisha kwenye kipindi cha pili kupitia mshambulizi Edinson Cavani.

Bao ya Cavani katika dakika ya 55 ilikuwa imerejesha matumaini ya klabu ya Manchester ambao ni mabingwa wa kombe hilo mwakani 2017 ila mechi hiyo ikaenda hadi kwa kwenye mikwaju ya penalti ambapo walipoteza vijana wa Ole Gunnar Solskjaer.

mlinda lango Geronimo Rulli aokoa mkwaju wa penalti
mlinda lango Geronimo Rulli aokoa mkwaju wa penalti
Image: Hisani

Mikwaju ishirini na moja ilifungwa huku Villarreal wakifunga 11 na Manchester United wakifunga 10 baada ya mlinda lango wake, David Degea kupoteza mukwaju wake na kuinyima klabu yangu kombe la pili la Europa.

Unai Emery
Unai Emery
Image: Hisani

Ushindi wa Vilarreal ulihakikishia mkufunzi Unai Emery kombe lake la nne kwenye ligi hiyo. Amefika fainali tano sasa huku akipoteza moja tu na klabu ya Arsenal mwakani 2019. Alishinda kombe tatu na klabu ya Sevilla mwakani 2014, 2015 n 2016.