Gwiji wa soka wa Italia Roberto Baggio avamiwa na majambazi

Staa huyo alivamiwa usiku wa Alhamisi alipokuwa akitazama mechi kati ya Italia na Uhispania,mashindano ya Euro 2024.

Muhtasari

•Staa wa zamani wa Italia,Roberto Baggio amejuruhiwa baada ya kuvamiwa na majambazi alipokuwa akitazama mechi kati ya Italia na Uhispania,Usiku wa Alhamisi.

•Mchezaji huyo amechezea vilabu kama Juventus ,AC Milan na Inter Milan akishinda mataji mawili ya Serie A kwa maisha yake.

Gwiji wa soka wa Italia
Roberto Baggio Gwiji wa soka wa Italia
Image: Hisani

Roberto Baggio alilazwa hospitalini kufuatia shambulio nyumbani kwake na majambazi waliojihami na kumfungia yeye na familia yake wakati wa mechi kati ya Uhispania na Italia usiku wa Alhamisi.

Gazeti la Corriere della Sera liliripoti kwamba familia ilikuwa ikitazama mechi ya Alhamisi usiku huko Altavilla Vicentina karibu na Venice wakati genge la watu watano lilipovamia mwendo wa saa 10 jioni.

Gwiji wa soka wa Italia, Baggio, aliyepewa jina la utani la 'The Divine Ponytail' enzi zake za uchezaji, inasemekana alipigwa kichwani alipokuwa akijaribu kupambana na wavamizi hao, ambao walimfungia yeye na familia yake kwenye chumba kabla ya kutoweka  na saa,  pesa na bidhaa nyingine za thamani.

Kulingana na ripoti za Telegraph  Baggio aliitoa familia yake chumbani baada ya majambazi hao kutoroka kabla ya kwenda hospitali kutibiwa jeraha lake la paji la uso .

Familia yake ilisemekana kutikiswa sana, lakini haikujeruhiwa, wakati wa wizi ambao ulikuwa chini ya uchunguzi wa polisi ulitoa picha za CCTV kusaidia uchunguzi wao.

Baggio pia alichezea vilabu vitatu vilivyopambwa zaidi vya Italia, Juventus, AC Milan na Inter Milan, akishinda mataji mawili ya Serie A katika maisha yake ya miaka 22.

Baada ya kustaafu soka, alikuwa afisa wa ngazi ya juu katika shirikisho la soka la Italia, akiongoza kitengo chake cha kiufundi. Lakini aliacha kazi mnamo 2013, baada ya miaka mitatu katika kazi hiyo, akishutumu bodi inayosimamia kwa kupuuza mapendekezo yake ya jinsi ya kukuza talanta za vijana.