Rais wa klabu ya Real Madrid ameongezewa mkataba katika klabu hiyo. Kura zilipigwa jana 19,Januari na akapita bila mshindani. mkataba wake mpya utakamilika mwaka 2029.
"kwa vile amepigania nafasi hiyo bila mshindani sasa namtangaza Perez kuwa rais wa Real Madrid," ilisema timu hiyo.
Real Madrid ilitangaza hili baya ushindi dhidi ya Las Palmas kwa mabao 4-1, ushindi huu uliwapa nafasi ya kupanda hadi kileleni mwa ligi ya La Liga.
Florentino Perez mwenye umri wa miaka 77 hajamenyana na mpinzani yeyote kwa chaguzi nne kufikia sasa ( 2013, 2017, 2021 na 2025) tangu kurudi katika klabu hio mwaka wa 2009 kwa mara ya pili.
Mfanyibiashara huyo maarufu huko Madrid alichaguliwa mara ya kwanza mwaka 2000 wakati Galactico alikua mmiliki wa klabu hio na akajiuzulu mwaka wa 2006.
Tangu urejeo wa Perez kama rais mwaka 2009, Real Madrid imeshinda mataji tano ya ligii ya Uhisipani na sita ya ligii uropa.