
Kocha Mikel
Arteta ametupilia mbali wazo la kumrudisha fowadi Raheem Sterling kwa Chelsea
ili kusajili mchezaji mwingine wa Premier League kwa mkopo.
Wanabunduki
wamepungukiwa katika nafasi ya mashambulio kufuatia majeraha mabaya waliyopata
Bukayo Saka na Gabriel Jesus.
Sterling
amekuwa na wakati mgumu kuonesha kiwango kizuri akiwa Arsenal baada ya kupewa
nafasi nyingi katika wiki za hivi majuzi na kufanya vibaya. Alitolewa tena katika
kipindi cha pili baada ya kuanzishwa katika mechi ya Jumatano dhidi ya Dinamo
Zagreb.
Huku
kipa Neto pia akiwa kwa mkopo kutoka Bournemouth, Arsenal haitaweza kuajiri
mchezaji mwingine wa Premier League kama suluhu la muda la masuala yao ya ushambuliaji
isipokuwa Mbrazil huyo, au Sterling, arejeshwe kwa vilabu vyao kabla ya muda
uliopangwa.
‘Hatufikirii
hilo,’ alisema Arteta ghafla alipoulizwa kama mojawapo ya mikataba ya sasa ya
mkopo ya Arsenal inaweza kukatizwa.
Huku
ikitarajiwa kuwa Bukayo Saka atarejea kabla ya mwisho wa msimu huu, kampeni ya
Gabriel Jesus 2024/25 imekamilika baada ya kufanyiwa upasuaji wa goti mapema
wiki hii.
Huku
Ethan Nwaneri akiwa amekosa michano minne kabla ya kurejea katikati ya wiki, Arteta
amekuwa akiwategemea sana Leandro Trossard na Gabriel Martinelli katika maeneo
mengi. Hii imeonyesha hitaji la wazi la mshambuliaji wa Arsenal haraka
iwezekanavyo.
Wanabunduki
wamehusishwa na wachezaji kadhaa mwezi huu lakini wachezaji kama Benjamin Sesko
na Alexander Isak wanaonekana kutokuwa na uwezekano wa kuhama Januari.
Matheus
Cunha, wakati huohuo, amekuwa na ofa nyingi na haijulikani anapendelea nini
huku Chelsea, Spurs na Nottingham Forest pia zikiwania saini yake.
Arteta
anasisitiza kuwa anataka kuimarisha chaguo zake huko Arsenal wakiwa bado
wanapigania taji la Ligi Kuu ya England na anatazamia kutinga hatua ya 16 bora
ya Ligi ya Mabingwa bila hitaji la mechi ya mtoano.
Kocha
huyo wa Arsenal tayari amekubali kuwa klabu yake inafanya kazi kutafuta
mchezaji mpya na kuweka wazi kuwa msajili mpya lazima akidhi vigezo fulani.
"Una rasilimali fulani, uwezo wa kuajiri wachezaji fulani, kukuza wachezaji fulani, kutumia wachezaji fulani kutoka akademi. Ni usawa wa kile tunachoweza kufanya," Arteta alisema.