logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Guardiola azungumzia Lewis-Skelly kudhihaki mtindo wa kusherehekea bao wa Haaland

Lewis-Skelly alitumia mtindo wa Haaland wa kusherehekea wa 'zen' baada ya kuifungia Arsenal bao la tatu.

image
na Samuel Mainajournalist

Football03 February 2025 - 07:39

Muhtasari


  • Mwezi Septemba, Haaland alimuuliza Lewis-Skelly "wewe ni nani?" wakati wachezaji wa Arsenal wakizozana na wa City.
  • Guardiola alitoa jibu tatanishi kuhusu Lewis-Skelly kuiga jinsi Erling Haaland husherehekea wakati wa mechi ya Jumapili.

Kocha Pep Guardiola alitoa jibu tatanishi kuhusu beki Myles Lewis-Skelly kuiga jinsi Erling Haaland husherehekea wakati wa mechi ya Jumapili ambapo Arsenal walishinda 5-1 dhidi ya Manchester City.

Kilikuwa kipigo kingine kikubwa katika msimu mmoja kwa City huku matumaini yao ya kubeba kombe la EPL kwa mara ya 5 mfululizo yakiendelea kufifia.

Wakati Erling Haaland alipoisawazishia City katika dakika ya 55 kwenye Uwanja wa Emirates, ilionekana kana kwamba mabingwa hao watetezi wangeweza kuendelea kuchukua pointi nyingi zaidi.

Hata hivyo, kiungo Thomas Partey alirejesha Arsenal uongozini ndani ya sekunde 40 baada ya mchuano kuanza tena, na kusababisha kuanguka kwa viwango vya City ambao walishuhudia Kai Havertz na vijana Myles Lewis-Skelly na Ethan Nwaneri wote wakilenga lango lao.

Lewis-Skelly ambaye wakati Man City ikimenyana na Arsenal kwenye Uwanja wa Etihad mwezi Septemba mwaka jana aliulizwa "wewe ni nani?" na Haaland, alisherehekea kwa kuonekana kumdhihaki mshambuliaji huyo kwa kufanya sherehe yake ya bao la 'zen'.

Akizungumza baada ya kumalizika kwa mchezo huo, Guardiola alisema: “Ninajutia dakika 25 tu zilizopita, tulisahau kufanya tulichopaswa kufanya, tulichofanya kwa dakika 65, 70.

Bila shaka ni mchezo mgumu kuanzia katika uwanja huu, dhidi ya timu hii kuanzia dakika za kwanza, imetokea mara nyingi msimu huu.

"Lakini baada ya dakika 10, 15, nadhani tulichukua mchezo na tukacheza vizuri sana, na tukawa ndani baada ya 1-1. Bila shaka 3-1 wakawa starehe, ni ngumu zaidi. Imetokea msimu mzima, tunatoa vitu vingi sana."

Guardiola alisema kuwa hakufahamu sherehe za Lewis-Skelly na aliulizwa kuhusu hilo wakati wa mkutano wake na waandishi wa habari baada ya mechi, ambapo alisema: "Oh, sikuiona. Sikuweza kufanya hivyo. Hiyo ni nzuri, hiyo nzuri."

Kisha kukawa na kimya cha muda mrefu, wakati huo Guardiola alitazama chini kwenye meza yake na kusema kimya kimya: "Hiyo ni nzuri."

Guardiola kisha akasimama na kumgeukia afisa wa habari wa City, na kusema: "Je, ulipenda jibu langu?"

Kipigo cha Jumapili kilikuwa mara ya 7 kwa vijana wa Guardiola kupoteza katika Ligi Kuu ya Uingereza msimu huu.

Kwa sasa wako katika nafasi ya nne wakiwa na pointi 41 kutoka kwa mechi 24 walizocheza msimu huu.

Makala Zinazohusiana


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved