logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Man United wafanikiwa kumshawishi chipukizi wa Arsenal kukataa mkataba mpya na kujiunga nao

United wanaripotiwa kukubali ada ya kumnunua kinda wa Arsenal Ayden Heaven katika dirisha la uhamisho wa Januari.

image
na Samuel Mainajournalist

Football28 January 2025 - 14:59

Muhtasari


  • Imeripotiwa kwamba beki huyo wa miaka 18 yuko tayari kufanya vipimo vya afya na Manchester United baada ya makubaliano kuafikiwa.
  • Frankfurt ya Ujerumani na miamba ya La Liga Barcelona pia walimtafuta Heaven huku Arsenal nao wakimpa mkataba mpya.


Manchester United wanaripotiwa kukubali ada ya kumnunua kinda wa Arsenal Ayden Heaven katika dirisha la uhamisho wa Januari.

Wiki iliyopita iliibuka kuwa United walifanya mawasiliano na Wanabunduki kumsajili beki huyo mwenye umri wa miaka 18 na walikuwa wakiongoza mbio za kumnasa kijana huyo.

Klabu ya Eintracht Frankfurt ya Ujerumani na miamba ya La Liga Barcelona pia walimtafuta Heaven huku Arsenal nao wakimpa mkataba mpya.

Lakini inaonekana sasa atajiunga na Wanabunduki huku vyanzo vya kuaminika nchini Uingereza vikiripoti kuwa makubaliano yamefanywa kati ya vilabu hivyo viwili.

Jarida la Athletic mnamo Jumanne asubuhi liliripoti kwamba mpango wa Heaven kutoka Arsenal kwenda United ‘unaendelea vyema’ huku masharti yake ya ufadhili wa masomo yakimalizika majira ya kiangazi.

Baadaye mchana, mwanahabari maarufu wa michezo Fabrizio Romano aliripoti kwamba beki huyo wa miaka 18 alikuwa tayari kufanya vipimo vya afya na Manchester United baada ya makubaliano kumalizika.

"Vipimo vya kiafya vimepangwa kwa (Ayden)baada ya kukataa mkataba mpya na Arsenal na Eintracht. Makubaliano yakiwa yametiwa muhuri rasmi,” Fabrizio alisema.

Mchezaji huyo wa kimataifa wa Uingereza wa Kikosi cha vijana wasiozidi miaka 19 alionekana Old Trafford siku ya Alhamisi, akitazama timu ya Ruben Amorim ikiishinda Rangers kwenye Ligi ya Europa.

Heaven alicheza mechi yake ya kwanza katika kikosi cha kwanza akiwa na Arsenal mapema msimu huu katika ushindi wa 3-0 wa Kombe la Carabao dhidi ya Preston mwezi Oktoba.

Ingawa bado hajaonekana kwenye Ligi ya Premia - meneja wa Arsenal Mikel Arteta hajaficha jinsi anavyoithamini Heaven - na amemjumuisha katika idadi ya vikosi vyake vya mechi za ligi kuu msimu huu.

Arteta alisifu Heaven baada ya kuanza na kucheza dakika 45 katika ushindi wa Arsenal wa kabla ya msimu mpya dhidi ya United kwenye Uwanja wa SoFi , jijini California mnamo Julai 28.

"Inavutia sana, sijui ni wachezaji wangapi wanaweza kufanya hivyo kwenye hatua kama hii katika umri wake," Arteta alisema kuhusu uchezaji wa Heaven.

Makala Zinazohusiana


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved