
Mashabiki wa soka kote ulimwenguni wanatarajia kwa hamu droo ya raundi ya 16 ya Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu wa 2024/25, itakayofanyika Ijumaa, tarehe 21 Februari 2025.
Droo hii itafanyika mwendo wa saa nane mchana kwa saa za Afrika Mashariki, katika Makao Makuu ya UEFA jijini Nyon, Uswisi.
Droo hii itaamua mechi zitakazoshuhudia timu 16 bora barani Ulaya zikipambana kwa nafasi ya kusonga mbele katika hatua ya robo fainali.
Baada ya hatua ya makundi kufikia tamati, timu zilizoshika nafasi za juu katika kila kundi zilifuzu moja kwa moja kwa raundi hii, huku nyingine zikilazimika kucheza mechi za mchujo ili kupata tiketi ya kuingia hatua ya mtoano.
Kwa mujibu wa sheria za UEFA, hakuna timu inayoweza kupangwa dhidi ya klabu iliyokuwa nayo kwenye kundi moja au timu kutoka taifa moja, jambo ambalo linafanya droo hii kuwa ya kusisimua zaidi huku baadhi ya miamba ya soka barani Ulaya ikiweza kukutana mapema kuliko ilivyotarajiwa.
Timu kama Real Madrid, Bayern Munich, Barcelona, na Liverpool zinatarajiwa kuonesha makali yao, huku miamba mingine kama Arsenal, Inter Milan, na Paris Saint-Germain wakisaka kutwaa taji hilo lenye hadhi kubwa barani Ulaya.
Timu Zilizofuzu kwa Raundi ya 16
Timu nane zilizomaliza juu katika hatua ya makundi na kufuzu moja kwa moja ni:
- · Arsenal
- · Aston Villa
- · Atlético Madrid
- · Barcelona
- · Inter Milan
- · Bayer Leverkusen
- · Lille
- ·
Liverpool
Timu hizi zitapangiwa kucheza dhidi ya washindi wa mechi za mchujo za hatua ya mtoano, ambazo ni:
- · Borussia Dortmund
- · Bayern Munich
- · Benfica
- · Club Brugge
- · Feyenoord
- · Paris Saint-Germain
- · PSV Eindhoven
- ·
Real Madrid
Uwezekano wa Mechi
Kulingana na kanuni za UEFA, timu zinaweza kupangwa dhidi ya klabu walizokutana nazo katika hatua ya makundi au kutoka nchi moja. Hapa chini ni orodha ya uwezekano wa mechi kwa kila timu:
Arsenal
Inaweza kucheza dhidi ya: Feyenoord, PSV Eindhoven
Aston Villa
Inaweza kucheza dhidi ya: Club Brugge, Borussia Dortmund
Atlético Madrid
Inaweza kucheza dhidi ya: Bayern Munich, Real Madrid
Inaweza kucheza dhidi ya: Benfica, Paris Saint-Germain
Inter Milan
Inaweza kucheza dhidi ya: Feyenoord, PSV Eindhoven
Bayer
Leverkusen
Inaweza kucheza dhidi ya: Bayern Munich, Real Madrid
Lille
Inaweza kucheza dhidi ya: Club Brugge, Borussia Dortmund
Liverpool
Inaweza kucheza dhidi ya: Benfica, Paris Saint-Germain
Mechi za raundi ya 16 zimepangwa kufanyika kama ifuatavyo:
Ø Wiki ya kwanza: 4/5 Machi 2025
Ø Wiki ya
pili: 11/12 Machi 2025
Huku timu zikijizatiti na kufanya maandalizi ya mwisho kuelekea hatua hii ya mtoano, mashabiki wanatarajia kuona mechi kali na za kusisimua zitakazotoa mwanga wa timu gani zina nafasi kubwa ya kutinga fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu huu.