logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Mikel Arteta awashutumu waamuzi wa EPL kwa maamuzi yao 'ya kupita kiasi'

Mkufunzi wa Arsenal Mikel Arteta ametilia shaka viwango vya maamuzi yanayofanywa na waamuzi akiyataja kuwa ya kupita kiasi

image
na Japheth Nyongesa

Football26 February 2025 - 16:25

Muhtasari


  • Declan Rice na Leandro Trossard pia walipokea kadi  nyekundu mapema msimu huu baada ya kupata kadi mbili za njano, ambazo zote zilijumuisha tahadhari.
  • Arteta, akizungumza kabla ya safari ya Gunners kwenda Nottingham Forest Jumatano, alidokeza kuwa sheria hizo hazijatekelezwa mara kwa mara wakati wote.

Mkufunzi wa timu ya Arsenal Mikel Arteta ametilia shaka viwango vya maamuzi yanayofanywa na waamuzi akiyataja kuwa ya kupita kiasi.

Kocha huyo alikuwa akizungumza akirejelea kadi nyekundu aliopokea mchezaji wake Myles Lewis - Skelly kwenye mchuano wao dhidi ya West Ham.

Lewis - Skelly alipokea kadi nyekundu moja kwa moja baada ya VAR kupendekeza kwamba mwamuzi Craig Pawson amtume beki huyo wa kushoto nje kwa kumunyima Mohamed Kudus fursa ya kufunga bao.

The Gunners walichapwa 1-0 nyumbani na West Ham United siku ya Jumamosi, kipigo chao cha kwanza katika uwanja wao wa nyumbani Emirates msimu wa 2024/25.

 Kufikia sasa hakuijakuwa na  maoni kwamba uamuzi wa Pawson haukuwa sahihi, lakini kadi nyekundu iliongeza idadi ya Arsenal kwa msimu wa Ligi Kuu ya England hadi tano - kiwango cha juu zaidi katika ligii.

Declan Rice na Leandro Trossard pia walipokea kadi  nyekundu mapema msimu huu baada ya kupata kadi mbili za njano, ambazo zote zilijumuisha tahadhari.

Arteta, akizungumza kabla ya safari ya Gunners kwenda Nottingham Forest Jumatano, alidokeza kuwa sheria hizo hazijatekelezwa mara kwa mara wakati wote.

"Ndio kuna vitu katika kadi nyekundu ambazo tulikuwa nazo ambazo tungefanya tofauti," Arteta alisema. "Ingawa sasa sheria zinaonekana kubadilika tena na haziendi jinsi ilivyokuwa hapo awali," alisema Arteta.

"Katika mambo mengine ni vigumu sana kubadilika kwa sababu unapomuuliza mchezaji kwa nini wamefanya uamuzi huo, ni uamuzi wa hiari sana. Harakati kali sana au maamuzi ambayo yalisababisha hatua hiyo. Ni vigumu sana kubadili hali hii," aliongeza.

Kocha huyo pia ameonesha imani kwa vijana wake huku akiwapongeza kwa kuwa na matokeo mazuri licha ya changamoto ambazo zimewakumba msimu huu.

"Tumepiga hatua kubwa msimu huu, wakati mkubwa, kwa sababu tunapaswa kuwa katika nafasi tofauti sana na kila kitu kilichotokea," Mhispania huyo aliongeza. "Hakuna timu katika historia ya Ligi Kuu ikiwa na kadi nyekundu tano na kiwango cha majeraha ambayo tumeyapata ambayo ingekuwa katika nafasi tuliyomo leo. Mnapaswa kuwa katikati ya jedwali na nje ya Ligi ya Mabingwa."

Arsenal kwa sasa wanawafuata viongozi wa ligii Liverpool ambao wako mbele kwa pointi 11 na wanajua kuwa kuna uwezekano mkubwa wa kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu England kuelekea Anfield kwa mara ya pili katika kipindi cha miaka mitano.

Makala Zinazohusiana


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved