logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Haaland Afichua Mke Wake Isabel Ndiye Aliyemtongoza Kwanza

Mshambuliaji wa Manchester City, Erling Haaland, hatimaye amevunja ukimya kuhusu safari ya mapenzi yake na Isabel Haugseng Johansen.

image
na Tony Mballa

Kandanda03 October 2025 - 13:54

Muhtasari


  • Erling Haaland afichua kuwa mpenzi wake Isabel Johansen ndiye aliyefanya hatua ya kwanza kwenye mapenzi yao, akieleza undani wa maisha yao ya familia na mapumziko.Mshambuliaji wa Manchester City, Erling Haaland, asema Isabel alimtuma ujumbe kwanza, akifichua maisha yao ya kifamilia, mtoto wao na upendo wa pamoja.

Nyota wa Manchester City na mshambuliaji hatari wa Ligi Kuu ya England, Erling Halaand, amefunguka kwa mara ya kwanza kuhusu uhusiano wake wa kimapenzi na Isabel Haugsen Johansen akieleza kuwa ndiye aliyechukua hatua ya kwanza ya kumtongoza.

Kauli hiyo aliitoa kupitia mahojiano na televisheni ya NRK nchini Norway, yaliyojikita kuhoji masuala ya kibinafsi ya watu mashuhuri.

Mshambuliaji wa klabu ya Manchester City Erling Haaland akisheherekea bao lake katika mechi iliyopita/ERLING HAALAND IG

Johansen Afanya Hatua ya Kwanza

Katika kipande cha mahojiano kilichotolewa kabla ya matangazo kamili, Haaland alieleza kuwa Johansen, ambaye walikutana katika klabu ya Bryne, ndiye alimwandikia ujumbe wa kwanza.

"Alinitumia ujumbe. Alicheza katika klabu moja na mimi, Bryne. Yeye ndiye aliyenichunguza. Si mimi niliyemchunguza," alisema Haaland.

Uhusiano wao ulianza wakati Haaland akiichezea Borussia Dortmund, huku Isabel akionekana mara kwa mara akimsapoti na kusafiri kuungana naye.

Safari Kutoka Bryne Hadi Manchester

Haaland alianza safari yake ya soka akiwa na umri wa miaka mitano katika akademi ya vijana ya Bryne FK.

Baada ya hapo, aliibukia RB Salzburg, akavuma Borussia Dortmund na sasa akawa nyota mkubwa katika Manchester City.

Johansen amekuwa sehemu muhimu ya safari hiyo, akishuhudia mafanikio makubwa yakiwemo makombe ya Premier League na Ligi ya Mabingwa.

Familia Yenye Furaha

Wapenzi hao walibarikiwa mtoto wao wa kwanza mwezi Desemba mwaka jana. Haaland alisimulia namna alivyopambana kufika kwa wakati kushuhudia uzazi huo, mara tu baada ya kumaliza mechi muhimu na Manchester City.

“Nilitoka uwanjani moja kwa moja kwenda kwake. Nilihakikisha nipo naye wakati wote,” alisema Haaland.

Mapenzi Yao ya Kawaida

Haaland alifichua kuwa maisha yao ya kimapenzi hayajafunikwa na fahari kubwa, bali yana ladha ya kawaida.

"Mimi kupika," alisema. "Wakati mwingine tunacheza Minecraft pamoja na kujenga nyumba. Au tunarudi Bryne na kuagiza kebabs."

Mshambuliaji huyo pia alitania kwamba kebab huenda zikawa chakula kitakachotumika hata kwenye harusi yao.

Isabel Johansen/ISABEL JOHANSEN IG

Johansen Akiwa Kwenye Jukwaa la Umaarufu

Wakati Haaland akizidi kutamba na rekodi za mabao, Johansen pia ameonekana mara nyingi kwenye sherehe za ushindi wa City.

Wawili hao waliandamana majira ya kiangazi huko Ibiza na pia walihudhuria maonyesho ya mitindo mjini Rome.

Mapenzi yao yameibua mazungumzo mitandaoni, wakipongezwa kwa kuendeleza uhusiano wa kudumu licha ya maisha ya umaarufu.

Mafanikio ya Haaland Uwanjani

Haaland ameanza msimu wa 2025/26 kwa kasi ya ajabu, akifunga mabao manane katika mechi sita za kwanza za Premier League.

Katika Ligi ya Mabingwa, alifikisha rekodi ya kuwa mchezaji wa haraka zaidi kufunga mabao 50 katika historia ya mashindano hayo.

Hadi sasa, ni Tottenham pekee walioweza kumzuia asifunge katika mchezo wa ligi. Hii imezidi kumthibitisha kama mmoja wa washambuliaji bora zaidi duniani.

Kwa kufichua upande wake wa maisha binafsi, Erling Haaland ameonyesha kuwa mbali na mabao na rekodi, yeye pia ni kijana wa kawaida anayependa mapenzi ya dhati na familia.

Safari yake na Isabel Johansen si tu hadithi ya kimapenzi, bali pia ni ushuhuda kwamba nyuma ya nyota wa soka, kuna maisha ya upendo na furaha ya kifamilia.

Isabel Johansen na Erling Haaland/ERLING HALAAND IG

Makala Zinazohusiana


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved