logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Fahamu Kwa nini Mbunge Peter Salasya Anataka Vijana Wote Wa Mumias East Waoe, Kwa nini Yeye Hataki Kuoa

Salasya ameweka wazi kuwa hayuko tayari kuingia kwa ndoa kwa sasa.

image
na Samuel Mainajournalist

Mahojiano13 February 2025 - 09:58

Muhtasari


  • Salasya alidai kuwa amewataka vijana katika eneobunge la Mumias Mashariki kuoa ili kuzuia uasherati na uhalifu katika eneo hilo.
  • Salasya alifichua kuwa ana mpango wa kuoa angalau wake watatu katika siku za usoni baaada ya kuhudumia watu wake.

Gidi, Salasya na Ghost katika studio za Radio Jambo

Mbunge wa eneo la Mumias Mashariki Peter Kalerwa Salasya ameweka wazi kuwa hayuko tayari kuingia kwa ndoa kwa sasa.

Akizungumza wakati wa mahojiano na watangazaji Gidi na Ghost, mwanasiasa huyo kijana alisema kuwa kwa sasa anajishughulisha na kuwafanyia kazi wapiga kura wake.

Hata hivyo alidai kuwa amewataka vijana katika eneobunge la Mumias Mashariki kuoa ili kuzuia uasherati na uhalifu katika eneo hilo.

“Mambo ya ndoa ni mambo ya Mwenyezi Mungu. Niliambia watu wa Mumias Mashariki kwamba wale vijana wote ambao wamebaleghe na kufikisha umri wa kuoa, waoe kwa sababu lazima kila mtu katika eneo bunge awe na majukumu. Wale vijana ambao wanasumbua ni wale ambao hawajaoa,” Salasya alisema.

Mbunge huyo kwa muhula wa kwanza alidai kuwa kuoa kwa sasa kunaweza kumfanya apoteze mwelekeo na kusahau jukumu kubwa la kuwahudumia wakazi wa eneo bunge la Mumias Mashariki ambalo analo.

 “Ndio maana nimesema kwamba mimi pekee ndiye nimeruhusiwa katika eneo bunge langu kutooa kwa sasa. Hii ni kwa sababu niko na kazi nyingi. Mimi ni mbunge ambaye nilipata watu wangu wakiwa nyuma sana, na lazima nitengeneze mambo hayo yote,” alisema.

“Nikiingia katika mambo ya wanawake, niingie katika mambo ya kuoa mabibi, nitakosa mwelekeo. Nimesema kwanza nipange eneo bunge, watoto wasome, watoto waanze kushika mwelekeo, nijenge mashule na mabarabara, madaraja, na kila kitu,” aliongeza.

Salasya hata hivyo alifichua kuwa ana mpango wa kuoa angalau wake watatu katika siku za usoni baaada ya kuhudumia watu wake.

“Mambo ikishaelekea sasa nitaambia watu wangu sasa nataka niwaletee mabibi watatu hapo mbele. Mipangilio itatokea, ratiba tutatoa, na nitawauliza ‘nyinyi kama wasichana ambao nimechagua, nataka niwaweke pamoja’. Wasichana ni wengi sasa kuliko wanaume. Lazima tukumbatie,” alisema.

Mbunge huyo kijana aliwataka wanawake wote ambao wamekuwa wakimmezea mate kuwa na subira kwani kwa sasa hapatikani.

Makala Zinazohusiana


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved