
MBUNGE wa Mumias Mashariki amewashanmgaza wafuasi wake kwenye mitandao ya kijamii baada ya kuonesha payslip ya mshahara wake wa mwezi Januari.
Kupitia kurasa zake mitandaoni, Salasya alichapisha picha ya payslip ya mshahara wake wa mwezi Januari kama mbunge ukiwa shilingi milioni 1.112 kabla ya makato.
Kilichowashangaza wengi, baada ya makato na tozo nyingi, mshahara wa Salasya alioupokea kwenye akaunti yake ulishuka hadi shilingi 18,746 pekee.
Mbunge huyo ambaye siku za hivi karibuni amekuwa mwiba mcungu katika wayo wa rais Ruto na serikali yake alilalamika vikali akisema kwamba licha ya hayo makato, bado mkuu wa taifa anatazamiwa kuongeza ushuru zaidi.
Salasya alionekana akiwahurumia wafanyikazi wengine wa serikali kama walimu wa mishahara ya chini akisema kwamba huenda wao wakapokea nunge kwenye akaunti zao baada ya makato.
“People have committed their payslips still Kasongo wants to add another deductions of NSSF sasa ya mwalimu na askari si itakuwa negative 10 😄🤣.Mungu tulikosea wapi tutubu ndio ukatupa kasongo kutesa sisi wafanyakazi 😄🤣😂The God of Abraham Isaac and Jacob have mercy on us now,” Salasya alionyesha mafadhaiko yake.
Wiki chache zilizopita wakati wa ziara ya wiki moja ya kimaendeleo ya rais katika ukanda wa magharibi mwa Kenya, mbunge huyo alikuwa miongoni mwa sauti chache zilizosimama kwa ujasiri na kumkosoa rais na sera zake.
Salasya alimwambia Ruto machoni kwamba miradi yake mingi haikuwa inafanya kazi kinyume na jinsi washauri wake walikuwa wanamwambia.
Mbunge huyo alimtaka rais kumwajiri kama mshauri wake ili awe anamwambia kile alichokitaja kuwa ni ukweli wa jinsi wananchi wa kawaida wanahisi kuhusu miradi yake kama mpango wa bima ya afya SHA na miradi mingine.