
Mangale kwenye mahojiano ya kipekee na Masawe Japani ndani ya Radio Jambo alikiri kwamba anajutia kutosoma wakati alikuwa na nafasi nzuri ya kukwamua maisha yake ya baadaye jambo lililomfanya kuishia kuwa kahaba.
Mama huyo alifichua kwamba aliponea kifo baada ya mwanaume aliyetaka kumuua kumueleza kwamba ameponea kwani miungu yake imekataa kafara ya damu yake hivyo akatupwa ndani ya msitu.
"Nilikaa miaka saba kwa ukahaba, nishaijaribu kuuliwa. Nilienda na mteja fulani, alitaka kunitoa kafara ila akanitupa ndani ya msitu wa Karura forest akaniambia miungu yangu imekukataa," alifichua mchungaji huyo.
"Alinichukuwa kwenye burudani, tukaongea mpaka bei na tukaingia kwa gari lake baada ya safari, sijui nini kiliingia akanitupa, kuna baridi kali, ni asubuhi na mapema, niko na skati fupi, nimetupwa. watu wakipita wanakuangalia," aliendelea.
Mangale pia ameeleza kwamba licha ya changamoto ambazo zilikuwa zinawakodolea macho hawakuwa tayari kuacha ukahaba hasa kutokana na ugumu wa maisha hasa baada ya kupitia mateso kutoka kwa wanaume wengine hivyo alikuwa anatafuta mbinu naye pia ya kulipiza kisasi.
"Tulikuwa tunafanya hayo kwa sababu ya hasira, Pia siku yako ikifika ya kudhulumu utambeba mpaka nguo zake ambazo amevaa mwilini hutaki kujua atatoka humo chumbani vipi," aliongeza.
"Mimi mara mingi nilikuwa na wazungu na ni wazuri sababu wanasema ukweli na pia wanatoboka, anaezakupea ata 50k, 20k na hajaenda na wewe. Nilikuwa Kahaba wa Mtaa na niko na boyfriend mtaani ," aliweka wazi.
'Kubadilika kwangu nilikuwa nimekaa mahali, pasta akanihubiria na akaniambia nimetumwa kwako na Yesu anataka kukutumia, na nikamuuliza Yesu anaeza okoa mtu kama mimi, mimi ni malaya, nimetoa mimba nimekosea vitu vingi. Baadaye nikaanza kusikia sauti ambazo si za kawaida kwa masikio yangu zikisema nataka kukutumia," Mchungaji huyo alieleza.
Mchungaji huyo alieleza kwamba kumchezea Mungu ni jambo baya kwani Mungu aliamua kumpa bwana ambaye ni mwizi mkubwa kwa sababu baada ya kumwambia yule pasta kwamba anataka bwana hakuwa tayari kubadilika lakini wakati aliamua kubadilika Mungu alimtendea makubwa
"Nilipata mume wangu mzuri ambaye tuko na yeye kwa sasa. Na nilipatana na yeye Facebook kama nahubiri injili, nikafanya harusi ya neti na nikaambia bwana yangu kuhusu siku zangu zilizopita na akaniambia usijali na mambo yaliyopita," Mangale alisema.