Samuel Mokonji ,22, kutoka Kiss alituma ujumbe akiomba kupatanishwa na mke wake Melvine Anyango ,20, ambaye hajaonana naye kwa miezi miwili iliyopita.
Samuel alisema ndoa yake ya chini ya mwaka mmoja ilivurugika miezi miwili iliyopita wakati mkewe alienda kumtembelea shangazi yake na hakuwahi kurudi.
"Tulikuwa kwa ndoa naye kwa mwaka mmoja alafu akapigiwa simu na mama yake aende kwa shangazi akamsalimie. Nikampa nauli akaenda. Baadaye akasema amechoka nimtumie nauli arudi. Kutuma nauli akablock namba yangu na hatujazungumza tena. Hata mama yake nampigia simu pia ni mteja," Samuel alisema.
Aliongeza, "Mahari nayo sijalipa. Tulikuwa tumepanga nilipe mwaka ujao. Yeye ni bibi yangu kwa sababu tumekaa naye kwa ndo mwaka moja. Naomba mnisaidie nijue uamuzi wake kama anarudi ili nijue vile tutakaa. Tulipata mtoto na yeye. Wakati mamake akisema amelemewa mahali nilikuwa natuma pesa. Kila kitu nilikuwa nampea, hakuna kitu alikuwa anakosa."
Melvine alipopigiwa simu alipuuzilia mbali madai ya kublock namba ya Samuel na kufichua kuwa alimwambia ana mpenzi mwingine.
"Sijablock namba yako. Ile siku si ulisema nisipige hiyo namba? Si uliniambia uko na mwingine," Melvine alisema.
Samuel alijitetea kwa kusema, "Hiyo ilikuwa ni hasira juu nilikuwa nimengoja urudi na hukuwa unakuja... Nilimngoja nikachoka nikampigia na namba ingine nikamwambia niko na mwingine."
Melvine aliendelea kubainisha kwamba tayari amezama kwenye mahusiano mapya.
"Na kama niko na mwingine? Sasa niko na mwanaume mwingine ambaye amenioa. Vile nilitoka huko ndio nilipata mpenzi mpya. Aliniambia ako mpenzi mpya na mimi pia nishapata," alisema.
Melvine pia alitoa ufichuzi wa kushtua kwamba Samuel sio baba wa mtoto wake.
"Mtoto sio wake. Sio wake. Mtoto nilipata kama nimeenda shule. Vile tulipatana na yeye, mtoto alikuwa mkubwa lakini sikuwa na mimba. Baba ya mtoto saa hii anafanya form four. Tulipatana na yeye kama niko na mtoto," alisema.
Samuel alisema, "Mtoto ni wangu lakini ni ile anakataa. Tulipatana na yeye akienda shule. Alafu nikamuoa.Tulikutana na yeye kama hana mtoto. Alisema nimempea mimba, akazaa nikajua ni wangu. Mtoto anafanana na mama yake."
Walipopewa fursa ya kuambiana maneno ya mwisho, Samuel alimwambia Melvine, "Nimeskia habari umeongea. Hata kama uliniacha sina ubaya na wewe. Mahali uko naomba uishi poa, sina ubaya na wewe."
Melvine alimwambia Samuel, "Asahau mtoto sio wake. Atafute wake. Sina maneno na yeye. Vile ako na huyo maisha yake iendelee tu poa."