Jamaa aliyejitambulisha kama Humphrey alituma ujumbe akiomba kupatanishwa na mke wake Ivyne ambaye alikosana naye mwezi uliopita.
Humprey alisema ndoa yake ilivurugika mwezi April wakati mpenzi wake wa zamani alipolala kwake baada ya mkewe kwenda nyumbani.
"Vile alienda, nilikuwa nimeachana na msichana. Huyo msichana aliniambia anataka kuenda kwao, akauliza kama anaweza kuleta mtoto. Alitaka tukutane mjini aone kama anaweza kuacha mtoto kwangu," Humphrey alisema.
Aliongeza, "Tulikutana mjini akasema anataka akuje nyumbani aone kama mke wangu atakubali aniletee mtoto. Nilimwambia mke wangu hayuko nyumbani akasema anataka twende nyumbani akathibitishe. Tulipofika akapata kweli mke wangu hayuko, akauliza kama anaweza kulala hapo na akaamua kulala. Kesho yake majirani walimuona wakamwambia. Aliniuliza kuhusu hilo nikamueleza, nilimwambia akasema hawezi kurudi hapo tena nimuoe huyo msichana tu. Alikuwa ananiambia tu nichukue huyo bibi nikae na yeye."
Ivyne alipopigiwa simu hakuwa na mengi ya kusema ila alikubali kumsamehe mumewe.
Alithibitisha madai ya mumewe na akasema atarudi kwa ndoa yake kwani tayari aliweza kumsamehe.
"Nitarudi. Nimemsamehea nitarudi," alisema.
Humphrey alisikika kuridhika na uamuzi wa mkewe kumsamehe.
Hajawahi kuniambia atarudi. Na kaka yake nikimpigia anasema nimpee muda," alisema.
Kuhusu uhusiano wake na mama mtoto, alisema, "Siwezi kujua kama mama mtoto ako mtu. Kama anataka mahitaji ya mtoto huwa namtumia. Alisema hataki kusikia maneno kama hayo mradi nishughulikie mtoto."
Je, una maoni gani kuhusu Patanisho ya leo?