
Maurice Masimba mwenye umri wa miaka 30 alituma ujumbe akiomba kupatanishwa na aliyekuwa mke wake Suzan Anjeche (29) ambaye alikosana naye takriban miaka mitatu iliyopita.
Maurice alisema ndoa yake ya miaka miwili ilivunjika Disemba 2022 baada ya mkewe kugundua ana mpango wa kando.
Alisema kuwa bado huwa anazungumza na mkewe huyo ila hawajaelewana kuhusu kurudiana.
”Tulikuwa tunazungumza wakati mwingine ikifika anakasirika tu. Niko na Imani bado huwa ananitambua juu juzijuzi tumeongea, jana na leo pia tumeongea. Ningependa mnisaidie juu akili yangu imesimama,” Maurice alisema.
Jamaa huyo alieleza kwamba alikatiza uhusiano na mpango wa kando baada ya kugundua kwamba ana mpenzi mwingine.
"Mpango wa kando, nilikuja kujua kuwa tunashare na askari fulani ambaye alikuwa anamtaka pia. Kwa hiyo tukaachana na yeye,” alisema.
Huku akieleza jinsi ndoa yake ilivyovunjika, Maurice alisema kwamba mpango wake wa kando alikuja kulala nyumbani kwake baada ya kutoka kumuona mpenzi wake, jambo ambalo hakufahamu na hakupangia.
“Bibi aliona huyo ni mpango wangu, keshoye akaamka akaenda. Alisema hiyo kitu hatawahi toa kwa roho na hatawahi kunisamehe,” alisema.
Kwa bahati mbaya, Maurice hakuweza kupatanishwa na mkewe kwani Suzan hakushika simu yake alipopigiwa.
Alipopewa fursa ya kumuongelesha mpenziwe hewani, Maurice alimwambia, "Nimeleta Patanisho kumuomba msamaha kwa yale yote nilimtendea. Mimi bado nampenda nay eye ndiye mwanamke wa ndoto zangu. Bila yeye sioni kama maisha yangu yanaenda mbele. Arudi tulee mtoto ambaye nilimpata naye, na tuzae wengine. Yeye ndiye kila kitu katika maisha yangu."
Je, una maoni ama ushauri gani kuhusu Patanisho ya leo?