
Phenny Anita 26 years kutoka Nairobi Chokaa, naomba kupatanishwa na Mchumba wangu anaitwa Job Aleisa 44 years, tulikua tumepanga kuoana ivi karibu na at the moment hata niko 3 months pregnant, lakini tumekosana makosa tu ndogo ndogo please tupatanishe please Giddy na Ghost
Mwanadada aliyejitambulisha kama Phenny Anita ,26, kutoka Nairobi alituma ujumbe akiomba kupatanishwa na mchumba wake Job Aleisa ,44, mbaye alikosana naye hivi majuzi.
Anita alisema uhusiano wao wa takriban miezi sita ulivunjika kufuatia mzozo wa kinyumbani uliotokea baada ya mtoto wake kuaga.
"Mtoto wangu alikufa nikaenda nyumbani. Nilipopigiwa kwamba mtoto amepata ajali, kuna pesa ilikuwa kwa nyumba. Nilichukua hiyo pesa nikakimbia nyumbani nikaenda matanga ya mtoto wangu.
Nilimwambia mume wangu kuna pesa ilikuwa kwa nyumba nimechukua nikakimbia nyumbani kuna kitu imefanyika. Nilimalizana na mambo na matanga nikarudi Nairobi tukasuluhisha maneno hadi tukarudiana vizuri," Anita alisimulia.
Alisema kwamba mzozo wao uliongezeka baada ya kumshuku mpenziwe kuwa na mpango wa kando.
"Baada ya hapo nikaenda kwake. Kuenda kwake ndio maneno ilianzia. Kuna msichana mwingine hapo jirani wake mwenye sijui ni kama walikuwa wanatongozan ama wanapiga tu stori nikachukulia ni kama wanatongozana.
Yeye ni mtu wa hasira, kumuuliza anasema tuachane. Yeye ako Kangemi nami niko Chokaa. Nilitaka nimuulize msimamo wake juu ata kukutana na mimi hataki. Kama haiwezekani niache kumsumbua. Ndo niko katika mwezi wa tatu wa ujauzito. Mtoto liyeaga alinipata naye. Alijua niko na mtoto mmoja," alisema.
Job alipopigiwa simu aliweka wazi kwamba tayari amekatiza uhusiano wake na Anita na akabainisha kwamba walizungumzia hilo.
"Huyo iliisha hivyo. Tumeongea kila kitu. Hiyo ni kitu alinimbia baada ya kuachana. Hakuwa ameniambia. Kama ako hivyo nilimwambia nitale mtoto. Tuliongea kila kitu. Wakati alishika mimba kwa nini hakusema. Lakini mtoto nitalea.Mimi ni Mluhya, Waluhya hawakataangi mtoto," Job alisema.
Anita alijibu, "Hiyo maneno tulishaongea hadi tukasuluhisha. Nilijua tutaendelea. Mimba nilipima baada ya kuachana. Wakati tulikuwa na yeye sikujua niko na mimba."
Hata hivyo, hakuwa na budi ila kukubali uamuzi wa mpenziwe.
"Mimi nilikuwa nkupenda bado hata kama hiyo maneno yote ilifanyika kati yetu. Mimi sikuwa na mtu mwingine isipokuwa wewe," Anita alimwambia Job.
Aidha, aliendelea kufunguka kuhusu masaibu ya mahusiano yao akisema, "Makosa yenye ilikuwa ni kuenda nyumbani bila kumwambia na kuchukua pesa bila kumwambia. Hiyo niliona ni makosa juu nilichukua hiyo pesa bila kumwambia. Kuna siku nilienda kwake nikampata na msichana kwa nyumba, sikuingia juu sikutaka kuleta vurugu nikalala kwa jirani. Keshoye nikaamka asubuhi nikaenda. Siku ingine nikamwambia niko hapo akaniambia nirudi mahali nimetoka hawezi toka nje. Tulikaa pamoja miezi kama sita tu."
Je, una maoni ama ushauri gani kuhusu Patanisho ya leo?