
Jamaa wa miaka 38 aliyejitambulisha kama Peter Ouma kutoka Ngong alituma ujumbe akiomba kupatanishwa na mke wake Trizah Ouma (24) ambaye alikosana naye mwishoni mwa mwaka jana.
Peter alisema ndoa yake ya miaka miwili ilisambaratika wakati mkewe alienda nyumbani mwezi Disemba na kukosa kurudi.
Hata hivyo, alikiri kuwa na wake wengine wanne kutoka mataifa tofauti ya Afrika Mashariki, jambo ambalo alishuku huenda lilivunja uhusiano wake na Trizah.
"Niko na wake watano. Nina umri wa miaka 38. Wa kwanza ni Mtanzania, wa pili ni Mganda, wa tatu ni Mburundi, na wa nne ni Mrwanda. Sasa huyu wa tano ndiye Mkenya. Hakujua yeye ndiye wa tano. Nashuku aliambiwa . Anajua ninaye mmoja tu," Peter alisema.
"Hao wake wanne niliwapanga kuna vile huwa wananilipa pesa kila mwezi. Niliwachukulia loan na nikawaambia watakuwa wananilipa. Sasa huwa wananilipa elfu kumi kila mwezi. Wote wako huku Kenya. Hao wengine wanajuana wote lakini hao wengine wanajuana. Huwa wanakutana na wanapendana sana. Hata wako na WhatsApp group. Mimi ni supervisor wa kampuni moja hapa Ngong," aliongeza.
Kuhusu jinsi Trizah alivyotoraka, Peter alisema, "Tulipanga aende tarehe 24 Disemba kupeleka sukari, hajawahi kurudi. Nilirudi nimechelewa alafu tukazozana. Niliskia fununu kwamba alienda ushago lakini sina uhakika. Nilitaka nataka kumuomba msamaha arudi tuendelee na maisha juu alienda na mtoto wangu na nampenda sana. Saa hii ata babake hapatikani kwa simu."
Juhudi za kumpatanisha Peter na mkewe hata hivyo ziligonga mwamba kwani Trizah alikataa kuzungumz aliposhika simu ya Gidi.
Wakati alipoulizwa sababu yake kuwa na wake wengi, Peter alisema, "Babu yangu alikuwa na wanawake 12. Hii uchumi nilikaa chini nikafanya hesabu zangu. Huwa sigharamiki sana. Wao ni wafanyibiashara. Niliwachukulia loan wakafungua biashara. Kila mwezi wananiptia Sh10k. Kila mwezi huwa tunakutana, inakuwa kama sherehe tunalala pamoja."
Alipopewa fursa ya kuzungumza na Trizah hewani, Peter alisema, "Triza tafadhali kama unaniskia sina ubaya na wewe. Mimi bado nakupend. Umeenda na mtoto na ningependa urudi tuishi pamoja. Kama nimekosea ningpenda kujua nirekebishe. Rudi tukae pamoja."