
Jamaa aliyejitambulisha kama Davy kutoka Elburgon alituma ujumbe akiomba kupatanishwa na mke wake Monica ambaye alikosana naye hivi majuzi.
Davy alisema ndoa yake ilisambaratika siku ya Jumapili wakati mkewe alitoroka kufuatia mzozo wa kinyumbani.
Alisema alizozana na mkewe baada ya kumshtumu kwa kutoka nje ya ndoa.
“Ilikuwa Ijumaa iliyopita, nilimuongelesha vibaya. Nilimwambia penye alikuwa alikuwa na mwaume mwingine. Naye akaniuliza “unadhani mimi ni Malaya”,” Davy alisimulia.
“Hatukuongeleshana wiki moja na sikuwa namuachia pesa ya chakula. Jumapili nilienda kazi kurudi nikapata amebeba vitu zake. Alibeba nguo zake, vyombo, vijiko, curtains, hata unga. Nilimpigia akaniambia ako mbali sana. Kufanya uchunguzi niliskia ako Elburgon lakini sina uhakika,” aliongeza.
Monica alipopigiwa simu, alifichua kwamba mumewe hajakuwa akitekeleza majukumu yake nyumbani.
Pia alimkashifu mumewe kwa kumshuku kukanyaga nje ya ndoa.
“Unajua, shida ya huyu kila wakati anapotelea majukumu yake, ukienda kujitafutia wewe mwenyewe ni shida hataki. Anasema umeenda kwa wanaume. Kama ni wewe utafanya nini na niko na mtoto? Anataka tu ukae hapo, na hapendi majukumu ya nyumba. Ukimwambia unataka hata chakula anasema hana pesa,” Monica alisema.
Davy alikiri makossa yake na akamuomba mzazi huyo mwezake amsamehe.
“Nilikuwa nagharamia kila kitu lakini Baada ya yeye kupata kazi ndiyo namwambia sina pesa,” alisema.
Monica hata hivyo aliweka wazi kwamba hawezi kurudi na kudai kwamba amechoka naye.
”Mimi huko kurudi hapana. Hatuwezani na wewe. Sijapata mtu mwingine na sitarajii kupata, lakini kwako hapana. Saa hizi nataka tu nikae maisha yangu. Wewe kaa maisha yako nami nikae maisha yangu,” alisema.
Aliendelea kufunguka kuhusu maovu ambayo mumewe huyo aliwahi kumfanyia ikiwemo kumfungia nje ya nyumba na kumkataa mtoto wao.
“Huyu hata kubadilika hawezi. Sio mara ya kwanza natoka huko. Kuna wakati alinifungia nje nikiwa na mtoto wa miezi mine. Ilikuwa usiku na kulikuwa kunanyesha. Alikuwa ndani na nilikuwa namuona. Alikuwa anasema mtoto mwenye niko naye sio wake, alikuwa anasema nimbadilisha hadi jina, nisimuite jina yake, nimpe jina la kwetu,” alisema.
Davy alibainisha kwamba anampenda mzazi huyo mwenzake na akamuomba ampe nafasi nyingine.
“Hiyo haiwezekani. Nimempea nafasi za kutosha. Saa hii hakuna nafasi ingine,” Monica alisema.
Davy alisema, “Kwa hayo yote naomba msamaha. Nimekubali makosa yangu. Arudi nyumbani na sitarudia makosa.”
Monica hata hivyo alisema, “Mimi sitaki. Kurudi nayo
siwezi. Sirudi nyuma tena, sasa nikusonga mbele. Vile alisema sio kumi mbili
kama wafuasi wa Yesu. Kwa hao kumi na mbili aende atafute atapata mmoja hapo. Aendelee
na maisha yake. Na mimi niendelee na yangu. Na aache kunisumbua kwa simu.”
Je. Una ushauri ama maoni gani kuhusu Patanisho ya leo?