logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Patanisho: "Ex Wangu Ameweka Profile ya Illuminati, Alinipea Siku 3 Za Kuishi Nafaa Nikufe Leo Valentines"- Joan

" Alinitumia meseji akiniambia sitaishi kwa Amani, nimekupea siku tatu ukufe. Hiyo siku ilikuwa leo," Joan alisema.

image
na Samuel Mainajournalist

Patanisho14 February 2025 - 09:35

Muhtasari


  • Mwanadada huyo alisema mumewe wa zamani alianza kumtishia baada ya kufahamu kwamba ameoleka kwingine.
  • “Haiwezekani, hadi ukufe uzikwe, siwezi nikakuachilia kitendo chenye ulinifanyia," Lazaro alisema.

Gidi na Ghost

Mwanadada aliyejitambulisha kama Joan Awuor (27) kutoka Ongata Rongai alituma ujumbe akiomba kupatanishwa na mume wake wa zamani Lazaro Ombayi (35) ambaye alitengana naye takriban miaka miwili iliyopita.

Joan alisema aligura ndoa yake ya miaka sita kufuatia mateso mengi ambayo Lazaro alikuwa akimpitishia.

Alisema hana nia ya kurudiana na jamaa huyo ila angependa kumuomba msamaha ili aache kumpa vitisho.

“Tuliishi na yeye lakini alikuwa ananitesa vibaya. Niliamua nitoke niende kwetu. Amenyamaza tu kwa mwaka mmoja hadi nikapata bwana mwingine. Tulipatana na huyo mzee na tunaishi  na yeye hadi saai,” Joan alisema.

Mwanadada huyo alisema mumewe wa zamani alianza kumtishia baada ya kufahamu kwamba ameoleka kwingine.

Dadangu mkubwa alimpigia ex wangu akamwambia niko na bwana mwingine na aachane na mimi niishi na Amani. Akiskia hivyo akaanza kunitumia meseji kwa WhatsApp hadi nikabadilisha namba. Alinitafuta kwa FB anaweka picha za Illuminati kwa profile yake. Alinitumia meseji akiniambia sitaishi kwa Amani, nimekupea siku tatu ukufe. Hiyo siku ilikuwa leo, ndio nafaa nikufe leo Friday. Nashangaa kwa anataka nini,” alisema.

“Niliangalia picha zake zenye amepost, anakaa ni kama ako na mwanake. Nilimwandikia meseji nikamwambia aishi na mwanamke ambaye ako na yeye. Aliniambia sitaishi na Amani, lazima ukufe ndio nitaishi kwa Amani. Nashindwa nilimfanyia nini, hadi saai niko mgonjwa nimelala tu hapa. Naumwa na kifua na kichwa,” aliongeza.

Lazaro alipopigiwa simu, Joan alichukua fursa kuomba msamaha na kumuomba aruhusu akae kwa amani.

“Nilikuwa nataka kukuomba msamaha. Kama nimekukosea naomba unisamehe na uniruhusu niishi na Amani kwa nyumba yangu. Sijui mbona unanifuatilia hivyo, inanikera sana. Uko na bibi na mimi niko na bwana,” alisema.

Lazaro hata hivyo alisikika kuwa na msimamo mkali na kukataa kumsamehe.

“Haiwezekani, hadi ukufe uzikwe, siwezi nikakuachilia kitendo chenye ulinifanyia. Nipatie mtoto wangu ukae na huyo bwana unaona ako juu. Nipatie mtoto wangu ukae na Amani,” Lazaro alisema.

Joan alimuuliza, “Unajua aje ni mtoto wako?”

Swali hili lilionekana kumkera sana Lazaro ambaye alisema, “Hakuna haja tuzungumze. Nimeachana na wewe!” kabla ya kukata simu.

Joan alilalamika kuhusu ukali wa mumewe huyo wa zamani na akaeleza chanzo.

“Juu ya ng’ombe tatu zenye alipeleka kwetu ndo maana anaongea hivyo. Huyo mtu ananitusi kweli kweli na inanikera,” alisema.

Alieleza kwamba watafanya mipango ya kurejesha ng’ombe ambazo Lazaro alimtolea.

“Watoto si wake. Anasema hivyo, akinipea mimba anasema sio yake. Mmoja ndio wake. Mwingine nilizaa kama niko nyumbani,” alisema.

Lazaro alipopigiwa simu kwa mara ya pili alisisitiza kwamba anataka tu mtoto wake.

“Huyo msichana mahali imefikia mimi nimemuachia mwenyezi  Mungu. Asiponirudishia mtoto wangu, huyo bwana ako naye ako na uwezo wa kuzalisha, akae naye sina shida. Mahari iende sina shida. Jamaa kunitusi kwa simu haitasaidia, hakuna meseji namkera nayo. Anirudishie mtoto akae na Amani,” alisema.

Aliongeza, “Aache matusi. Ata kama amepata bwana mzuri, akae na bwanake sina shida, lakini achukue mtoto wangu anipatie. Nataka tu mtoto wangu nikae na yeye, sina haraka na kuoa. Aache kusema mtoto sio wangu, hiyo ndiyo ananikera nayo. Hii maneno tumeachia Mwenyezi Mungu. Akiamua kuenda na mtoto bas, ni sawa.”

Gidi alipomshauri, alikubali kumuachilia mtoto iila akamtaka Joan aache madharau.

“Sawa, nimemuachilia hata mtoto akae naye. Achunge ulimi yake. Madharau tu asinionyeshe. Mi namuomba Mwenyezi Mungu mwenyewe aamulie haya maneno. Mimi sio mganga ama mchawi,” alisema.

Katika maneno yake ya mwisho, Joan alisema, “Aache kunitumia meseji kwa FB na aache niishi kwa Amani."

Lazaro kwa upande wake alisema, “Aache kutafuta marafiki zangu akiuliza kama nishakufa aje anizike.”

Makala Zinazohusiana


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved