
Jamaa aliyejitambulisha kama Godian Omusi (28) kutoka Busia alituma ujumbe akiomba kupatanishwa na aliyekuwa mchumba wake Elizabeth Okumu (27) ambaye alikosana naye takriban miaka mitatu iliyopita.
Godian alisema shida iliingia kwenye uhusiano wake wa miaka mitatu iliyopita wakati Elizabeth alifunga safari kuenda Uarabuni.
Alikiri kwamba mpenziwe alimuongeza kwenye kundi la WhatsApp la wanadada ambapo alianza kuchat na marafiki zake.
“Huyu mwanadada tulipokutana 2019, tukawa kwenye mahusiano kidogo hadi 2022. Ilifika mahali akasema anataka kujoin college. Wakati huo akasema juu sina uwezo aende uarabuni. Aliniadd kwenye Whatsapp group ya madame wanafanya kazi pale, nikaanza kuchangia pale ikaleta shida,. Nilitaka nijue hali iko vipi huko,” Godian alisema.
“Alipata naanza kuchat na marafiki zake. Hapo ikaleta shida. Tukaunda group ingine hapa Kenya na familia yake na mashemeji wake, tukasuluhisha hayo maneno. . Shetani ndiye aliniingia kidogo nikaanza kuchat na hao madame. Baadaye akaniblock kila mahali,” aliongeza.
Godian alieleza wasiwasi wake kwamba amepata taarifa kuwa mchumba wake tayari amerudi nchini na ameolewa kwingine.
“Miezi miwili iliyopita nilipata taarifa kwamba amerudi. Hivi majuzi binamu yake aliniambia ni kama ameolewa . Alinipromise nisioe. Sasa ameniweka, nataka kujua kama alioolewa. Akiskia tu sauti yangu anablock. Sasa amerudi sasa amekaa miezi miwili. Kuna binamu aliniambia aliolewa, kuna mwingine ananiambia ako Nairobi bado,” alisema.
Elizabeth alipopigiwa simu, alikata ghafla baada ya kuskia ni Patanisho.
Godian alikiri kwamba ni ngumu kukubali kwamba mchumba huyo wake wa zamani hamtaki tena baada ya kutoka Saudia.
“Ni ngumu kukubali. Ni mtu ambaye nimetambulisha nyumbani, ni mtu tunajuana vizuri. Vile alienda uarabuni ni mimi na mamake tu tulijua. Hakuwa ameambia mtu yeyote. Itabidi tu nikubali juu sina cha kufanya,” alisema.
Alipopewa fursa ya kusema maneno ya mwisho kwa Elizabeth, Godian alisikika kumlaani mpenziwe huyo wa zamani akimwambia kwamba atamtafuta tu.
“Pesa ya Muarabu huisha. Utanitafuta tu. Ama utaolewa kwa bwana ya mtu. Itafika mahali utupwe kama mzigo ya kuibwa. Ama utapewa mimba na uachwe. Utashtuka ukipelekwe nyumbani upate wewe ni bibi wa tatu. Hiyo nusu mita umekuja nayo itafika mahali iishe. Pesa ya Mwarabu inakimbia kama points za Liverpool,” Godian alisema.
Je, una ushauri
ama maoni gani kuhusu Patanisho ya leo?