
Joseph Ombogi (32) kutoka Kisii alituma ujumbe akiomba kupatanishwa na mke wake Martha Kemunto (28) ambaye alikosana naye takriban miaka mine iliyopita.
Joseph alisema ndoa yake ya miaka kumi ilisambaratika mwaka wa 2021 wakati mkewe alitoroka kutokana na ulevi wake na tabia ya kuenda nje ya ndoa.
“Niliangia kwa ndoa 2012 nikaoa huyo mwanamke tukaishi vizuri lakini masaibu yalianza vile nililipa mahari kwani baadae niliingia kwenye uraibu wa pombe na nikatoka nje ya ndoa. Ile kugongana yangu na yeye haikuleta amani. Hatukuwa tunaskizana kabiasa na mimi mambo ya pombe nikazama kabisa,” Joseph alisimulia.
Alisema ulevi wake uliendelea kukithiri adi mkewe akachoka naye.
“Ilfika mahali akaniacha. Akaniambia nitafute mke mwingine ambaye ataweza kunivumilia. Mpaka aliniachia watoto wetu wawili. Nikijaribu kuongea na yeye anakuja juu anasema mimi na yeye ni kwisha. Watoto wako na mama yangu, huwa naskia anawapigia simu lakini hajawahi kuniambia. Nimejaribu kumuomba msamaha ananiambia it is over, ako na mtu mwingine ambaye anampenda zaidi,” alisema.
Licha ya kuwa wametengana kwa muda na hata Martha kumwambia tayari yuko na mtu mwingine, Joseph alisisitiza kwamba angependa kuomba msamaha ili mzazi huyo mwenzake ajue anampenda.
Martha alipopigiwa simu hata hivyo, aliweka wazi kwamba uhusiano wake na Joseph ulifika kikomo na hana nia ya kurudi.
Aidha, alifichua maovu ambayo mzazi huyo mwenzake alimfanyia ikiwemo kwenda nje ya ndoa na kumpiga.
“Mwambie iliisha tu hivyo. Ni stori mob. Kazi ni ulevi na wanawake. Mwambie hakuna haja,” Martha alisema.
“Huwa naskia lakini unaambia mtu sana na hataki kubadilika. Ukipenda mtu sana ndo anaanza madharau, hakuna haja. Unajua mtu akikwambia atakuua, kinachofuata si ni hiyo. Mimi nishawahi enda mpaka hospitali nikawekewa maji juu ya yeye kunipiga kwa hiyo hakuna haja. Kama ni watoto mimi hushughulikia. Huwa naongea na mamake,” alisema.
Alipoulizwa kama amepata mtu mwingine, alisema, “Hii ni town!”
Aliongeza, “Sitaki kuongea na yeye. Mimi nilimwambia atafute
mtu mwingine. Ukishaongea na mtu mara ya kwanza akose kuskia, hakuna haja ya
mara pili. Nishamwambia, yeye haelewi. Kama sina feelings kwa mtu, nitafanya
nini? Hakuna haja ya kuforce issues.”
Joseph hata hivyo alitaka kujua kama mzazi huyo mwenzake tayari amemfahamisha mpenzi wake wa sasa kwamba amelipiwa mahari.
“Huyu mtu anasema ako na yeye, ashamueleza yeye ni mwanamke wa mtu na ashalipiwa mahari? Nataka kumuuliza kama huyo mtu anaelewa ameacha watoto sehemu,” Joseph alihoji.
Martha alijibu, “Hii ni town, kesi baadaye.”
“Mimi huenda kwao kama hayuko nafanya shopping na nakaa na wao. Nikiambia mtu afanye hivi hataki kubadilika, hakuna haja. Saai tungekuwa mbali, lakini hataki kuskia,” Martha aliongeza.
Joseph alijibu, “Najuta na ndio maana nikaleta Patanisho.”
Martha aliendelea kufichua maovu ya mumewe, na kueleza jinsi alivyomuonyesha madharau kwa nyumba.
“Ata kama mtu ako na mpango wa kando huwa anaficha. Sio kuonyesha mke wako. Sasa unachukua simu unavideo call mtu kama umetoa nguo na mke wako ako hapo. Hiyo ndo nini? Yeye Akipata pesa hivi, ni wanawake,” alisema.
Joseph alisema, “Kama ameamua ni hivyo, maisha ni yake. Mimi nilikuwa naomba msamaha. Nimeridhika na maamuzi yake lakini hakuna kitu ameongea hapo. Hajaamua uamuzi ulio sawa kulingana na mimi.”
Martha alisema, “Mimi sina ubaya na wewe kwa sababu huwa tunaongea. By the way huwa ameoa. Mwanamke alikuja akaenda. Alikuwa amewekwa hapo kama matatu tu.”
“Alijitakia yeye mwenyewe. Apambane na hali yake. Na akipata mtu abadilishe tabia kwa sababu tunapenda kubembelezwa na mambo matamu matamu. Ashaharibu kila kitu,” alimalizia kwa kusema.