
Sharon Mboone mwenye umri wa miaka 24 kutoka Kisumu alituma ujumbe akiomba kupatanishwa na mama mkwe wake Doreen Anyango ambaye alikosana naye mwaka jana..
Sharon alisema uhusiano wake na mama mkwe uliharibika Septemba mwaka jana wakati alimuandikia jumbe mbaya baada ya mumewe kumuacha na kuoa msichana mwingine.
Alisema wakati alikuwa mjamzito alikuwa anabishana na mumewe hadi akaondoka kwenda nyumbani na akaoa msichana mwingine.
“Kwa sasa tuko na huyo kijana tunaishi pamoja Kisumu. Tulikosana na kijana, tulikuwa tunabishana kidogo wakati nilikuwa na mimba. Mimba haikumpenda sana hatukuwa tunaskilizana. ILikuwa tu ugomvi kwa nyumba kila saa. Ikafika mahali akaenda nyumbani,” Sharon alisimulia.
“Nilikuwa naishi na ndugu na beshte mwingine hapo. Akaambia ndugu yake anaenda nyumbani kukaa kwa muda hujulikani. Vile alienda akatuma ndugu yake aniambie ameenda nyumbani kuoa msichana mwingine, kama nitakubali nikae na kama sitaki niende,” aliongeza.
Sharon alisema ni baada ya kupata taarifa kwamba mumewe anaoa msichana mwingine ambapo aliamua kumtusi mama mkwe.
“Wakati huo nilikuwa na mimba ya miezi tisa, nikapigia mama mkwe kumuuliza. Akaniambia hizo maneno hajui na hataki kuingilia. Niliskia uchungu kwa sababu alikuwa ameniacha kwa nyumba na ameniachia 1500. Niliamua kuandikia mama mkwe meseji mbaya. Nilimwambia nishawahi kuona mama mkwe wabaya lakini sijawahi ona mama kama wewe. Nilikasirika kwa sababu nilikuwa nampigia simu hashiki. Nilikuwa nimetumia pesa zikaisha,” alisema.
“Haikuwa vitisho kwamba angeoa msichana mwingine. Alienda akamuoa baada ya wiki mbili alileta huyo msichana Kisumu, akamtafutia nyumba ingine, alikuwa anakuja mpaka kwa nyumba yangu. Ilibidi nikubali lakini hatimaye aliachana na yeye. Huyo msichana hakukaa. Yule alitaka mimi nitoke yeye abaki,” aliongeza.
Bi Doreen alipopigiwa simu alisikika kuwa mgumu kumsamahe mke huyo wa mwanawe.
Alifichua matusi ambayo mwanadada huyo alimtupia na kusema itakuwa ngumu kuelewana.
“Huyo msichana nilikuwa nampenda sana. Amenikosea makossa ambayo ata siwezi nikamsamehe. Vile walipatana na kijana wangu akaja nyumnbani nikamkaribisha. Vile walikosana alijua makossa ni yangu. Akaanza kinutusi akisema eti mimi ndiye nimemfanya kijana wangu akaoa msichana mwingine. Mimi sikujua,” Bi Doreen alisema.
“Huyo msichana vile aliskia kijana wangu amekuja na msichana mwingine nyumbani aliniandikia meseji mbaya. Alidhani mimi ndiye nimepatia kijana msichana mwingine. Niliambia kijana asifukuze huyo msichana mwingine. Mimi nimekuwa kama adui kwake. Sijui tutafanya aje juu mimi siwezi nikamsamehe
Mimi ndiye nimefanya akaishi na huyo bwanake. Wakikosana mimi nagombanisha kijana wangu sio yeye. Makosa yangu iko wapi inafanya msichana ananitusi hivyo. Sio mara ya kwanza. Sijawahi kumwambia asikuje hapa kwangu. Ni msichana wa kijana wangu lakini asiwahi kuniomba msamaha. Siwezi kumsamehe,” aliongeza.
Sharon alimwambia, “Ningependa afungue roho anisamehe.”
Bi Doreen alimwambia, “Si wewe ndiye ulisema hutakanyaga kwangu tena? Niliforwadia mamako. Hapo nilikosea nini?”
Sharon hata hivyo aliendelea kiomba msamaha na kueleza majuto yake.
Mimi najua nilikosa. Ningependa unisamehe. Mimi nilijua vile Brian alikuja eti wewe ndiye umemtafutia msichana Mimi naomba tu unisamehe tu. Ata kama sitakuja nyumbani. Hakuna haja nikae na kijana na hatuelewani na mama mkwe,” Sharon alisema.
Hatimaye Bi Doreen alikubali kuyeyusha roho na kumsamahe Sharon, jambo lililozua hisia nzito za furaha.
"Mimi ndiye niliambia Brian asikufukuze. Sharon nimekukosea nini jameni ikafanya unitusi hivyo? Ebu waambie.. Lakini mimi ni Mkristo, nimeokoka lakini nimemsamehe, akuje nyumbani na asiwahi kitu kama hiyo,” alisema.
Gidi ambaye alisikika kujawa na bashasha alisema, “Amen. Nimetoa machozi kwa sababu ya vile umemsamehe Sharon. Hiyo kitu imemsumbua roho.”
“Akuje nyumbani. Alete mtoto nyumbani,” Bi Doreen alisema.
Sharon alimalizia kwa kusema, “Nimefurahi aki umenisamehe mama. Nitamheshimu. Hakuna siku ingine nitawahi kumtumia meseji.”
Je, una ushauri ama maoni gani kuhusu Patanisho ya leo?