Kuku wakiwa wengi wanamwaya mtama, siri zao zikiwachoma na kusindwa kuziweka huwa wanatoboa katika kipindi cha toboa siri.
Mwanamke mmoja aliwaacha mashabiki wa radiojambo midomo wazi baada ya kutoboa siri, jinsi mama mkwe wake amekuwa akimpa kazi ya uchawi.
Kulingana na mwanamke huyo ambaye alidai kwamba ametoka katika kaunti ya Kisii alisema kwamba mumewe na wachawi wengine wamekuwa wakimpa kazi ya kupika uji na ugali.
Hii hapa siri yake;
"Nataka kumwambia mama mkwe na mume wangu kwamba nimechoka na hiyo kazi yao ya uchawi, nimekuwa nikiwapikia ugali na nyama ya mtu usiku wanakula na wachawi wenzao
Pia wamefuga fisi ambao nimekuwa nikiwapikia uji, ni fisi wawili wa kiume na wa kike, sasa nimechoka nataka kuwatobolee siri kwama nimechoka na kazi yao na kwamba nitawaacha."