In Summary

•Mchekeshaji huyo ambaye pia ni muuguzi amedai kwamba amekuwa akipokea jumbe nyingi kutoka kwa wanadada wanaomezea mate kupachikwa ujauzito naye.

•Hata hivyo ameamua kuvunja nyoyo za wanadada hao kwani ametangaza hana nia ya kutimiza maombi yao

David Oyando almaarufu kama Mulamwah
Image: INSTAGRAM

Takriban mwezi mmoja unusu baada ya Mulamwah kukaribisha kifungua mimba wake duniani, mchekeshaji huyo sasa ametoa madai kuwa wanatamani kupata mtoto pamoja naye.

Kupitia kurasa zake za mitandao ya kijamii, mchekeshaji huyo ambaye pia ni muuguzi amedai kwamba amekuwa akipokea jumbe nyingi kutoka kwa wanadada wanaomezea mate kupachikwa ujauzito naye.

"Wanadada wengi wananitumia jumbe wakitaka kupata watoto nami" Mulamwah amedai.

Hata hivyo ameamua kuvunja nyoyo za wanadada hao kwani ametangaza hana nia ya kuwatimizia maombi yao.

Ujumbe huo wa baba huyo wa mtoto mmoja umeibua gumzo kubwa mitandaoni wengi wakionekana kuwa na ushauri wa kumpatia msanii huyo.

@Mwendiajnr Wanataka pesa zako kaka

@Githui_254 Tafadhali watume kwa DM yangu, pia mimi sina masikio

@ukonangapi Unaringa kuhusunini jamaa

@fanuel_ Kutafuta kiki ni ugonjwa!

Mulamwah pamoja na mpenzi wake Carrol Sonnie walibarikiwa na mtoto wa kike, Keilah Oyando mnamo Septemba 20.

"Na ni msichana. Muujiza umewasili.. maneno hayaweza kueleza ninavyohisi, ni kitu cha maana zaidi kuwahi fanyika maishani mwangu. Karibu kipenzi @keilah_oyando" Mulamwah aliandika kwenye ukurasa wake wa Instagram mtoto alipozaliwa.

Mchekeshaji huyo alieleza raha kubwa  ambayo alipata moyoni baada ya kubarikiwa na mtoto wake wa kwanza  huku akidai kuwa siku itimiapo ataonyesha urembo wa bintiye hadharani.

"Ni mrembo, siwezi subiri kuonyesha walimwengu siku moja na niwe na mazungumzo ya baba na binti. Mimi ni baba mwenye raha. Shukran kwa Mungu" Alisema Mulamwah.

View Comments