In Summary

• Mcheshi Erick Omondi amekashifiwa kwa kula uroda na msichana katika hoteli moja jijini Nairobi halafu akakosa kutimiza ahadi ya kulipa binti huyo shilingi elfu ishirii na tano.

• Hata hivyo ni zaidi ya mwaka mmoja sasa na Erick Omondi hajaweza kutimiza ahadi yake , jambo lililomlazimu manzi wa TRM kuchapisha ujumbe katika mtandao wa Instagram kumsuta Erick Omondi kwa kuwa mdanganyifu na kukosa kuchukua simu zake alipompigia.

Eric Omondi
Image: INSTAGRAM// ERIC OMONDI

Mcheshi Erick Omondi amekashifiwa kwa kula uroda na msichana katika hoteli moja jijini Nairobi halafu akakosa kutimiza ahadi ya kulipa binti huyo shilingi elfu ishirii na tano.

Akizungumza na chombo kimoja cha habari, msichana huyu almaarufu manzi wa TRM alisema kwamba alikutana na Omondi katika sehemu moja ya kujistarehesha halafu baadaye mcheshi huyo akamuomba wakatulie katika hoteli ya kifahari mjini ili kujuana zaidi.

Manzi wa TRM anasema kwamba siku hiyo Erick Omondi alisema alikosa kwenda nyumbani kwa kile alichokitaja kuwa kulikuwa na aila yake pale na hivyo hawangepata muda mzuri wa kutangamana na kidosho huyo.

Aidha, binti huyo alikiri kwamba alimwelezea Omondi kwamba ana changamoto ya kulipa ada ya sehemu alimokuwa akiishi, huku rais huyo wa ucheshi akiahidi kugharamikia ada hiyo ambayo ilikuwa takribani shilingi elfu ishirini na tano.

Hata hivyo ni zaidi ya mwaka mmoja sasa na Erick Omondi hajaweza kutimiza ahadi yake , jambo lililomlazimu manzi wa TRM kuchapisha ujumbe katika mtandao wa Instagram kumsuta Erick Omondi kwa kuwa mdanganyifu na kukosa kuchukua simu zake alipompigia.

Kwa sasa inasubiriwa kuona iwapo Omondi atafanya kweli na kulipa deni.

View Comments