Msanii wa miziki ya injili, Ekodydda ametangaza rasmi azma kuwani kiti cha uwakilishi wadi katika eneo la Mathare kaskazini katika uchaguzi mkuu ujao.
Kupitia ujumbe aliochapisha katika ukurasa wake wa Instagram, Ekodydda amewarai wakazi wa eneo hilo kujisajili kama wapiga kura ili kwa pamoja waweze kuleta maendeleo katika eneo hilo.
Hata hivyo, msanii huyo amesema kwamba hana hela za kugawa wananchi ila anaamini kwamba Mungu atamsaidia kunyakua kiti hicho.
“Sina pesa ya kuwapa watu ama chama kubwa, lakini nakuja kwenu kwa jina la Mungu. Mwakilishi wadi wa eneo la Mathare kaskazini, chukua kura sasa tubadilishe mitaa,” Ekodydda aliandika.