Sina pesa ila naomba mnichague kama 'MCA' - Ekodydda

Muhtasari

• Msanii wa miziki ya injili, Ekodydda ametangaza rasmi azma yakle ya kuwani kiti cha uwakilishi wadi  katika eneo la Mathare kaskazini katika uchaguzi mkuu ujao.

• Hata hivyo, msanii huyo amesema kwamba hana hela za kupeana kwa wananchi ila anaamini kwamba Mungu atamsaidia kunyakua kiti hicho.

Ekodydda
Ekodydda
Image: Instagram, KWA HISANI

Msanii wa miziki ya injili, Ekodydda ametangaza rasmi azma kuwani kiti cha uwakilishi wadi  katika eneo la Mathare kaskazini katika uchaguzi mkuu ujao.

Kupitia ujumbe aliochapisha katika ukurasa wake wa Instagram, Ekodydda amewarai wakazi wa eneo hilo kujisajili kama wapiga kura ili kwa pamoja waweze kuleta maendeleo katika eneo hilo.

Hata hivyo, msanii huyo amesema kwamba hana hela za kugawa wananchi ila anaamini kwamba Mungu atamsaidia kunyakua kiti hicho.

“Sina pesa ya kuwapa watu ama chama kubwa, lakini nakuja kwenu kwa jina la Mungu. Mwakilishi wadi wa eneo la Mathare kaskazini, chukua kura sasa tubadilishe mitaa,” Ekodydda aliandika.

Ikumbukwe kwamba msanii huyo kwa siku nyingi sasa amekuwa katika mstari wa mbele kupigania wananchi wa kawaida na kuitaka serikali kusapoti talanta za vijana wengi humu nchini.

Hatua hii ya Ekodydda inajiri kipindi ambacho wasanii wengi wameonekana kujitosa katika kivumbi cha chaguzi zijazo wakiahidi kubadilisha mambo na kuwasaidia vijana wenzao.