In Summary

• French Montana amelalama hatua ya Instagram kumfungia Kanye West Instagram yake.

• Amesema msanii huyo yumo mbioni kuanzisha mtandao wake wa kijamii.

Kanye West na mshikaji wake French Montana
Image: TMZ (Instagram), French Montana (Twitter)

Baada ya staa wa hiphop kutokan Marekani kuonekana kupoteza marafiki wengi kutokana na mzozo wa kutalikiana na mpenziwe wa muda mrefu Kim Kardashian, msanii huyo pia mapema leo amefungiwa instagram yake.

Rafiki wake wa karibu French Montana amekuwa miongoni mwa watu wa kwanza kutoa tathmini yao kuhusu hatua hiyo ambayo instagram walichukua, kwa kile walisema Kanye West alitumia maneno ya ubaguzi wa rangi dhidi ya Trevoh Noah.

French Montana ameonekana kumtetea mshikaji wake Kanye West na kusema kwamba instagram hawakufaa kumfungia akaunti yake.

Wamemfungia Mshikaji Wangu Kanye West Kutumia Instagram. Yupo Mbioni Kutengeneza Mtandao Wake Mwenyewe,” aliandika Montana kwenye Twitter yake.

TWITTER

Pia alifichua kwamba huenda Kanye West yuko mbioni kuanzisha mtandao wake mwenyewe kwa kile kinachoonekana kama kutuma ujumbe unaosema mitandao iliyopo ya kijamii haina uhuru kwa watumizi wake.

Ikumbukwe Kanye miezi miwili iliyipita alitangaza kufungua jukwaa lake binafsi la kusambaza miziki baada ya kudai kwamba majukwaa yaliyopo yanawakandamiza wasanii.

Kama maneno ya Montana ni kweli, basi Kanye West akajiunga katika orodha ya watu wanaotaka kufungua mitandao yao baada ya kuhisi kuhujumiwa na mitandao iliyopo.

Aliyekuwa rais wa Marekani Donald Trump pia alianzisha mtandao wake kwa jina Truth Social, baada ya kufungiwa na Facebook na YouTube kwa kile mamlaka za mitandao hiyo zilisema ni kusambaza madai ya uongo kuhusu uchaguzi wa Marwkani na virusi vya Corona.

Ushikaji wa French Montana umedumu kwa muda mrefu mpaka ilifikia kipindi siku chache zilizopita ambapo Kanye West aliapa kumfanya French Montana bilionea.

View Comments