In Summary

• Mchekeshaji Trevoh Noah ametoa tamko lake baada ya Kanye West kuondolewa katika orodha yqa watakaotumbuiza kwenye hafla ya Grammy kwa ubaguzi wa rangi dhidi ya Noah.

• Trevoh Noah amesikitika na kusema kwamba hakusema Kanye West aondolewe bai alitaka tu apewe ushauri nasaha.

Image: GETTY IMAGES

Kitumbua cha staa wa hiphop kutoka Marekani Kanye West kinazidi kuzama mchangani hata zaidi huku majanga yakimwandama na kumganda kama ruba.

Hii ni baada ya kutoa kauli za kumbagua mchekeshaji Trevoh Noah kwenye Instagram yake na kupelekea kufungiwa kwa saa 24.

Taarifa mpya sasa ni kwamba msanii huyo amefungiwa nje ya ku-perform katika tuzo za Grammy kwa matamshi yake ya ubaguzi wa rangi dhidi ya Trevoh Noah.

Ikumbukwe Trevoh Noah ndiye ameratibiwa kuwa kuongoza hafla ya Grammy itakayofanyika Aprili 3.

Trevoh Noah hatimaye amelizungumzia hilo na kuonesha kutoridhika kwake na hatua ya wandaaji wa Grammy kumuondoa Kanye West kutoka katika orodha ya watumbuizaji, kisa kumdhalilisha yeye kwa maneno ya ubaguzi wa rangi.

“Nilisema mmshauri Kanye West, sikusema mumuondoe katika orodha ya watumbuizaji,” aliandika Trevoh Noah kupitia Twitter.

Kampeni za kumdumaza Kanye katika mitandao ya kijamii zimeendelezwa na watu ambao wanashinikiza mitandao hiyo kumfungia akaunti zake kwa kile wanasema ni kuandika mambo ya kudhalilisha watu wanaotofautiana naye katika kauli.

Kuna uvumi pia kwamba kampeni zimeoteshwa mitandaoni watu wakitaka Kanye West kuondolewa katika orodha ya watakaotumbuiza kwenye tamasha la Coachela.

View Comments