In Summary

• Mwanablogu mtata Vincent Mboya amesema kwamba Bahati hawezi kushinda uchaguzi wa eneobunge la Mathare.

• Alisema kwamba hamchukii Bahati, ila tabia zake haziwezi kumruhusu kuwa mbunge wa eneo hilo.

Image: HISANI

Mwanablogu matata nchini, Vincent Mboya amesema kwamba msanii Kevin Kioko almaarufu Bahati hawezi kuwa mbunge wa eneo la Mathare.

Akizungumza kupitia video aliyoipakia katika akaunti yake ya YouTube, Mboya alisema kwamba Bahati hana sifa za kuwa kiongozi.

" Bahati labda awe mbunge wa Mathare Mental hospital," Mboya alisema.

Mboya alisema kwamba Bahati amedorora kimuziki na anataka kujitosa katika siasa ili kujikomboa kimaisha.

Aidha , Mboya alitilia shaka kwamba Bahati hajapata masomo ya chuo kikuu, akitaja kwamba hicho ni moja kati ya vigezo vinavyoangaliwa kabla ya mtu yeyote kujitosa katika kinyang'anyiro cha ubunge.

Pia alimkashifu mwanamuziki huyo akisema kwamba huwa anaiga mambo kutoka kwa msanii mwenzake, Willy Paul.

Alishikilia kwamba Bahati aliamua kufanya kibao na kinara wa ODM Raila Odinga baada ya kupata taarifa kwamba Pozze pia alikuwa amepanga kuachia kibao na kiongozi huyo.

Alikiri kwamba Bahati amekuwa akifanya kiki nyingi, ambazo kulingana naye hazifai kufanywa na mtu ambaye analenga kuingia katika nafasi ya uongozi.

Alimtaka msanii huyo kuzingatia kufufua kipaji chake cha muziki, badala ya kujitosa katika siasa ambapo hawezi kupata ushindi.

Mboya alisema kwamba Bahati hapaswi kufikiria kwamba ufuasi wake katika mitandao ya kijamii utaendana na kura.

View Comments