In Summary

• Pritty Vishy alipakia video katika Instastory yake na keleza jinsi mambo yalivyokuwa alipokuwa shule ya upili.

Aliyekuwa mpenzi wa msanii Simple Boy, Pritty Vishy alizungumzia maisha yake alipokuwa shule ya upili.

Vishy alisema kwamba alikuwa mwanafunzi pekee aliyekuwa na mwili mkubwa shuleni mwao, jambo ambalo lilimpa kiburi.

Alipakia video katika Instastory zake iliyoonyesha wakati alipokuwa shule ya upili na nguo rasmi za rangi ya nyeupe na samawati.

"Mtambue binti yenu, nilikuwa mnene kiasi cha kuwaogofya walimu na hata waliogopa kuniadhibu kama walivyokuwa wakiadhibu wanafunzi wengine," Pritty Vishy alisema.

Hata hivyo, Vishy alifichua kuwa hakupenda kuashiriwa kuwa mnene au mtu kukejeli mwili wake.

Vishy hakutaja kuwa mwenye haja na masomo ila alitaja mambo yaliyomvutia katika shule ya upili.

Alisema kuwa alikuwa na majina ya majazi kwa sababu ya kuwa na tabia ya kuwasimanga wanafunzi wengine.

"Naapa, nilikuwa napenda shule kwa sababu ya chakula cha shule na kuwanyanyasa wengine, ungeniita mnene tungepatana kotini. Nilikuwa mkubwa hata kuliko walimu wangu," alisema.

Miezi kadhaa iliyopita, aliyekuwa mpenzi wa Pritty Vishy ,Simple Boy alifichua kuwa walikuwa wamekubaliana na Vishy kufunga ndoa baada ya kumaliza masomo yake ya shule ya upili.

Binti huyo alikuwa kwenye mahusiano na mwanamuziki Simple Boy kwa muda kabla ya kuvunja uhusiano huo.

Simple Boy alisema kuwa alikutana na mpenzi huyo wake wa kitambo alipokuwa darasa la nane.

Pritty Vishy alikuwa amedai kuwa alimwacha Simple Boy kwa kuwa hakuwa anajisimamia katika uamuzi wa muziki wake.

Jambo hilo lilimpa Pritty Vishy fikra za kuwa Simple Boy hangeweza kujiamulia mambo mengine kando na muziki wake hata katika mahusiano yao.

 

View Comments