In Summary
•Benson Njiru (22) na Emmanuel Mutura (19) ambao walikuwa wanafunzi katika chuo kikuu cha Kabarak na chuo cha mafunzo ya kiteknolojia cha Don Bosco mtawalia wanadaiwa kutoweka baada ya kukamatwa na polisi kutoka kituo cha polisi cha Manyatta mnamo Julai 1.
•Juhudi za kuwatafuta zilinoga kwa kipindi cha siku tatu zilizofuata hadi miili yao ikapatikana katika chumba cha kuhifadhi maiti cha Embu Level 5 mnamo Jumanne wiki iliyopita.
•Wanamitandao waliojawa na ghadhabu kufuatia kukithiri kwa ripoti za matendo ya kikatili miongoni mwa maafisa wa usalama wameungana na familia ya marehemu kwenye vita ya kutafuta haki.