In Summary

•Mamlaka imeonyesha wasiwasi juu ya watu wenye silaha ambao walikuwa wanapambana na polisi.

•Kamishna wa eneo la Bonde la Ufa,George Natembeya amedai wavamizi hao wana bunduki aina ya M16 , ambazo haziuzwi nchini humo.

Image: BBC

Mamia ya watu wamekimbia makazi yao wakati ghasia zilipotokea katika hifadhi ya Laikipia iliyopo bonde la Ufa nchini Kenya.

Mamlaka imeonyesha wasiwasi juu ya watu wenye silaha ambao walikuwa wanapambana na polisi.

Zaidi ya watu 12 wameuawa, wakiwemo sita waliouawa wiki jana

Milio ya risasi ilisikika majira ya mchana, moshi ukionekana huku polisi wakisema ghala la shule moja liliteketea na wanafanya uchunguzi kuhusu tukio hilo .Kupitia taarifa polisi wamesema wanafunzi hawakuwa katika shule hiyo ya Merigwiti iliyodaiwa kuchomwa katika ripoti za vyombo vya habari hapo awali nchini humo .

Wakazi wamekuwa wanakimbia makazi yao ambayo wamekaa kwa miongo kadhaa.

Washambuliaji katika hifadhi binafsi ya Laikipia pia wanalisha mifugo yao kwa jeuri kwenye mashamba ya mahindi ya wakulima wasio na ulinzi.

Kamishna wa eneo la Bonde la Ufa,George Natembeya amedai wavamizi hao wana bunduki aina ya M16 , ambazo haziuzwi nchini humo.

Polisi wa Kenya huwa wanatumia bunduki za G3 na AK47, ambapo mara nyingine watu wasiokuwa na vibali hutumia kufanya ujambazi.Wamesema wanaendelea na oparesheni ya kurejesha utulivu

View Comments