In Summary

•George Ouma anaripotiwa kuingia nyumbani kwa mwanamke huyo katika kijiji cha Esikulu mwendo wa saa kumi na mbili jioni ya Jumatano baada ya kuona aliyekuwa anamtunza ameondoka.

•Mhasiriwa alipiga nduru katika juhudi za kuomba usaidizi kutoka kwa wapita njia huku mshukiwa akiendelea kutosheleza kiu chake cha tendo la ndoa.

crime scene
Image: HISANI

Jamaa mmoja amelazwa katika hospitali ya Busia baada ya kupatiwa kichapo cha mbwa na umati wenye ghadhabu kufuatia madai ya kubaka mwanamke mwenye ulemavu wa mwili.

George Ouma anaripotiwa kuingia nyumbani kwa mwanamke huyo katika kijiji cha Esikulu mwendo wa saa kumi na mbili jioni ya Jumatano baada ya kuona aliyekuwa anamtunza ameondoka.

Kulingana na DCI, mshukiwa alipothibitisha kwamba mwanamke yule alikuwa peke yake alichukua fursa hiyo kutosheleza kiu chake cha tendo la ndoa bila idhini.

Mhasiriwa alipiga nduru katika juhudi za kuomba usaidizi kutoka kwa wapita njia huku mshukiwa akiendelea kujitosheleza.

Kwa bahati nzuri ndugu ya mwanamke huyo ambaye alikuwa ameenda sokoni alirejea na kumpata akiwa anatenda kitendo kile cha unyama.

Ndugu ya mhasiriwa alishirikiana na wanakijiji wengine kumwadhibu mshukiwa kwa mateke, ngumi na silaha mbalimbali kabla ya polisi waliokuwa karibu kufika na kumuokoa kabla hajakata roho.

Polisi walimkimbiza Ouma katika hospitali ya kaunti ya Busia kupokea matibabu kabla ya kufikishwa mahakamani na kushtakiwa kwa kosa la ubakaji.

View Comments