In Summary

•Katibu Mkuu Wizara ya Afya  Susan Mochache  ambaye alikuwa ni  mgeni mkuu  wakati wa uzinduzi huo

•Gavana wa Kaunti ya Meru Kiraitu Murungi ambaye pia alihudhuria hafla hiyo alisema kuwa Mahakama inafaa kuwa  makini na kutoa adhabu kali kwa wahusika

Mwanamke mwenye huzuni
Image: HISANI

Kaunti ya Meru imeorodheshwa katika nambari ya tatu kwa visa vya ukatili wa kijinsia na mimba za mapema  miongoni mwa Vijana, hii ni kulingana na afisa mkuu wa Afya ya umma John Inanga.

Haya iliwekwa wazi na mkuu huyo wakati  alikuwa akizungumza katika chuo cha Mafunzo  ya  ualimu Meru katika hafla ya uzinduzi wa kampeni ya kupinga ukatili wa kijinsia na mimba za  mapema dhidi ya  vijana katika Kaunti hiyo.

''Ukatili wa Kijinsia, maambukizi ya  Virusi  vya Ukimwi na mimba za mapema ni shida kubwa sana hapa, ni jambo ya kushangaza''  Inanga alisema.

Pia aliongeza kuwa wanafanya kila juhudi  zinazopaswa kuchukuliwa ili kupunguza viwango vya juu vya maambukizi  ya Virusi vya Ukumwi, na Ukatili wa Kijinsia.

Katibu Mkuu Wizara ya Afya  Susan Mochache  ambaye alikuwa ni  mgeni mkuu  wakati wa uzinduzi huo aliwarai Viongozi wa Siasa na washikadau wa Serikali kukuwa mstari wa mbele kuhamashisha umma kuhusu jinsi ya kuepukana na changamoto hizo. 

''Visa vya  maambukizi ya  Ukimwi vimeongezeka, watu wengi wamesahau kuchukua tahadhari juu ya maambukizi hiyo ,badala yake  wanazingatia namna ya  kujikinga dhidi Janga la Korona kuliko ugonjwa wa Ukimwi'' Mochache alisema.

Gavana wa Kaunti ya Meru Kiraitu Murungi ambaye pia alihudhuria hafla hiyo alisema kuwa Mahakama inafaa kuwa  makini na kutoa adhabu kali kwa wahusika wanaoeneza  Ukatili wa Kijinsia badala ya kuwawacha  kwa dhamana.

''Mimba za mapema miongoni mwa Vijana ni kwasababu ya Ukatili wa Kijinsia  ambapo pia huchangia pakubwa kwa  usambazi wa Ugonjwa wa Ukimwi miongoni mwa Vijana,'' Kiraitu  alisema.

View Comments