In Summary

•Kutokana na notisi hiyo, walimu hao wote waliondolewa kwenye orodha Juni 22, mwaka huu.

Mkurugenzi Mtendaji wa Tume ya Utumishi wa Walimu Nancy Macharia.
Image: STAR

Baadhi ya walimu 73 hawataruhusiwa kutoa huduma zao katika taasisi yoyote ya mafunzo.

Haya ni kulingana na ilani ya Tume ya Kuajiri Walimu iliyochapisha orodha ya walimu 73 walioathiriwa.

"Kulingana na kifungu cha 30 cha Sheria ya TSC (2012), Tume inapendekeza  kuchapisha majina ya walimu ambao wameondolewa kwenye Rejista ya Walimu," notisi hiyo ilisema.

Kulingana na Sheria ya TSC, kuna sababu tano ambazo zinaweza kusababisha mwalimu kuondolewa kwenye sajili.

Baadhi ya sababu ni pamoja na; ikiwa mwalimu amekufa, Tume isiporidhika  jinsi mwalimu alipata usajili uenda ni kwa njia za udanganyifu na ikiwa mtu amepatikana kujihusishwa kimapenzi na mwanafunzi.

Kama wametiwa hatiani kwa kosa la jinai ambalo kwa maoni ya Tume linamfanya mtu huyo kuwa hafai kuwa mwalimu; (e) ambaye Tume imeagiza aondolewe kwa sababu ya taratibu za kinidhamu,” kipenge cha  Sheria hiyo.

“Iwapo watapatwa na maradhi hayo ya kimwili au kiakili au udhaifu ambao unamfanya mtu huyo kushindwa kutekeleza majukumu ya ualimu, kuondolewa,''

Sheria pia inaelekeza kuwa TSC itachapisha jina na maelezo ya mwalimu ndani ya mwezi mmoja baada ya kuondolewa

"Endapo jina la mwalimu yeyote litaondolewa kwenye usajili chini ya Sheria hii, jina hilo halitarejeshwa isipokuwa kwa maelekezo ya Tume."

Zaidi ya hayo, mwalimu ambaye jina lake limeondolewa kwenye sajili ya TSC atakoma kuhudumu kama mwalimu kuanzia tarehe ya kuondolewa.

 

View Comments