Baba yangu aliamini kuwa ninataka kuwa mchekeshaji aliponiona kwa gazeti-Mulamwah
- Mwaka jana Mulamwah alivuma kwenye mitandao ya kijamii baada ya kutoka kwenye tasnia ya burudani
Katika kitengo cha ilikuaje tulikuwa naye mchekeshaji David Oyando almaarufu Kendrick Mulamwah ambaye aliweka mambo kadha wa kadha wazi.
Mwaka jana Mulamwah alivuma kwenye mitandao ya kijamii baada ya kutoka kwenye tasnia ya burudani.
"Nilianza kukajeliwa kwenye mitandao ya kijamii ya twitter ambapo wanamitandao walikuwa wanakejeli kila kitu kunihusu
Ukianza kukejeliwa kwenye mitandao ya twitter hapo ni kama umeingia jehenamu, baada ya kejeli hizo nilipatwa na msongo wa mawazo," Alieleza Mulamwah.
Huku akizungumza kazi yake ambayo alisome chuo kikuu alisema,
"Nilisomea kazi ya uuguzi, mimi ni muuguzi baada ya kumaliza masomo yangu niliendaa katika hospitali kuu ya Kenyatta kwa mafunzo
Baba yangu hakupendezwa na hatua yangu ya kuwa mchekeshaji, wakati mmoja aliamka na kuniona kwa gazetti, na nikaanza kuanya mabadiliko nyumbani, hapo ndipo aliamini kwamba napenda kazi ya uchekeshaji
Aliniambia kama nataka kuwa mchekeshaji haya ni sawa," Alisema.
Mulamwah alisema kwamba kazi ya muuguzi ni nyingi sana na hana wakati wa kutumia pesa zake licha ya wauguzi wengi kuwa na pesa.