
MBUNGE wa Mumias Mashariki Peter Salasya amewakosha watumizi wa mitandao ya kijamii baada ya kuonyesha muonekano wake mpya kwenye video fupi aliyopichapisha.
Katika video hiyo, Mbunge huyo anayejitambulisha kama ‘Gen Z’
alionesha video hiyo akiwa amevimba midomo na kufichua kwamba alifanyiwa
upasuaji.
Salasya alitania kwamba ndio ameanza safari ya kupata nafuu
baada ya upasuaji mdogo kwenye midomo yake na kutania kwamba midomo yake sasa
imekuwa mikubwa kama ya mwanashosholaiti Fulani kutoka Tanzania.
“Ndio naendelea kupata nafuu baada ya upasuaji mdogo wa midomo. Sasa hivi midomo yangu inakaa kama ya yule Mrembo wa Tanzania, Madonna,” alisema.
Hata hivyo, baadhi walihisi kwamba alikuwa anamrejelea Mrembo
wa huku Kenya Tanasha Donna ambaye mwaka jana alionyesha muonekano wake mpya
baada ya kuboresha muonekano wa midomo yake.
Wengine walihisi kwamba mbunge huyo alikuwa anazua utani tu
kwa kutumia teknolojia za kisasa kama vile akili mnemba (AI) kuhariri muonekano
wake, wakihisi kwamba sio kweli kuhusu kufanya sajari ya midomo.
Kwa mujibu wa Cleveland Clinic, Upasuaji wa midomo maarufu
kama ‘Lip Augmentation’ huongeza unene kwa midomo nyembamba, na kuunda kuonekana
zaidi kwa ujana.
Kuna aina kadhaa za kuongeza midomo, ikiwa ni pamoja na
kujaza midomo, vipandikizi, uhamisho wa mafuta na kuinua midomo. Wakati wa
kurejesha, matokeo na hatari zinazowezekana hutofautiana kwa kila utaratibu.