
SIKU moja baada ya uvumi wa DJ Mo na mkewe Size 8 kufanya harusi ya kisiri katika Maeneo ya Sigona kaunti ya Kiambu, mchungaji Size 8 amevunja kimya kuhusu tukio hilo.
Kupitia ukurasa wake wa Facebook, Size 8 alifichua kwamba
tukio hilo lilikuwa kufanya upya viapo vyao vya ndoa mnamo Februari 18.
Mchungaji Size 8 alimshukuru Mungu kwa matukio yote ambayo
yametukia katika uhusiano wao wa zaidi ya miaka 10 sasa.
“Siku hii ❤️18:02:25 ❤️Mungu alifanya hivyo na
tukafanya upya viapo vyetu vya ndoa 💍 .....kwa neema na rehema
za Mungu tumeona urejesho wa Mungu katika ndoa yetu.....kile ambacho Mungu
hawezi kufanya hakipo.....Je, hili ndilo tendo la Bwana, nalo ni la ajabu
machoni petu......."
Japo ilikuwa harusi ya kisiri, Size 8 alisema mashabiki wake
watapata nafasi ya kipekee kuona matukio hayo kwenye YouTube Alhamisi hii.”
“Kesho kwenye youtube ya
murayas tunayofuraha kukushirikisha video ya yale Mungu amefanya...mtu
asherehekee jina la Yesu Kristo pamoja nasi.... uuuuuwwiii haleluya...... Yesu
Kristo ni Bwana!” Size 8 alichapisha.
Sherehe ya harusi ilipambwa na marafiki zao wa karibu na
familia ambao wote walikuwa katika shangwe huku wawili hao wakila kiapo cha
harusi.
Miongoni mwa walioonekana kwenye harusi hiyo ni watu
mashuhuri kutoka tasnia ya kidunia na ya injili.
Wageni wa harusi walikuwa wamevaa nguo nyeusi. DJ Mo alikuwa
amevalia suti nyeupe huku Size 8 akitamba na gauni zuri la Light-pink.
Harusi hiyo imekuja siku chache baada ya DJ Mo na Size 8
kuweka hadharani kuwa wamerudiana baada ya kuachana kwao kulikotangazwa mwaka
jana.