
MWANAMKE mmoja mwenye umri wa makamo amezua gumzo katika mitandao wa X baada ya kuibua tetesi kwamba wanaume wanaojua kupika kuwa nao katika mahusiano ni kujikosea heshima kama mwanamke.
Katika video hiyo ambayo imegawanya wachangiani maoni kwa
makundi mawili, Mrembo huyo alianza akisema kwamba anawaonea huruma sana
wanawake walioko kwenye mahusiano ya kimapenzi na wanaume ambao ni wapishi
wazuri.
Kwa mjibu wa mwanadada huyo, mwanamume yeyote ambaye ni fundi
katika masuala ya jikoni ni ‘red flag’ kubwa sana, akisema kuwa hao mara nyingi
ndio huwa sumu kuishi nao.
“Unapoolewa na mwanamume
anayeweza kupika ni red flag. Wakati nyinyi mnapigana, atapika, atakula,
atafurahi na kwenda kulala.”
“Hakuna kisingizio cha
yeye kukubembeleza. Hasa ikiwa anaweza kupika zaidi yako na pia kujua jinsi ya
kuweka ubaya, utateseka katika uhusiano huo,” alisema.
Aliongeza akitoa onyo kwa wanawake kutofanya uthubutu wa
kuolewa na mwanamume anayejua kupika, akiita hatua hiyo kama moja kati ya
makosa makubwa ambayo mwanamke yeyote anayejipenda atafanya.
Mwenyewe, alisema kuwa hawezi kubali posa kwa mwanamume
anayejua kupika hata kwa mtutu wa bunduki.
“Usijaribu kuingia katika
uhusiano na mwanamume anayejua kupika, hata mimi mwenyewe siwezi kubali
mwanamume wangu awe hodari jikoni. Kupika ni biashara yangu tu,” aliongeza.
Tazama video hiyo hapa chini jinsi watu waliweza kuchangia maoni kwenye jambo hilo;